Aliyeposa Kisha Akahutumiwa Kuwa Kambaka Mtoto
SW
Asalaam alayku ama baada ya kumshuru Allah Subuhana Huwataala na kutakia rehma Mtume wetu Muhammad Salallah Alayhi Wasalaam. Napenda kuwatakia kila la kheri waislamu wote wa ujumla.
Swali langu lipo hapa me nina jamaa yangu alikuwa nataka kufunga ndoa na jamaa mmoja hivi yaani huyo bwana harusi ni jamaa
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu posa, harusi na kubaka. Hakika mara nyingi huwa tunajitia katika shida kwa kushindwa au kutotaka kufuata maagizo ya kisheria. Kitendo cha uzinzi (zinaa) si kitendo kidogo katika sheria yetu na sheria hakuacha mlango huo kwa dhana na fikra zetu. Mwanzo tayari kuna utata
Ama katika sheria, kitendo cha zinaa ni lazima kishuhudiwe na Waislamu wane, waadilifu, walio baleghe na wenye akili timamu. Ikiwa itakuwa wamepatikana hao, tatizo na utata wote utaondoka. Ikiwa hakuna ushahidi huo basi huyo kijana hana hatia yoyote. Tunaomba kila mmoja awe ni mwenye kusoma tafsiri ya Suratun Nuur (24): 1 – 10, kwa maagizo na mafunzo mengi ndani yake.
Kuondosha utata, huyo bwana anaweza kuozeshwa huyo msichana. Na ikiwa familia ya msichana pamoja na msichana mwenyewe amekuwa hataki tena kuolewa na huyo kijana, inabidi harusi hiyo ivunjwe na huyo kijana arudishiwe pesa zake na pia uhasama usiwepo.
Kwa kuwa sisi tuko mbali hatuwezi kusema zaidi ya hayo. Kwa kupata ufumbuzi wa hayo, inabidi kesi hiyo ipelekwe kwa Qaadhi kama wapo sehemu mnayoishi. Ikiwa hawapo basi pateni Shaykh mwadilifu ili aweze kuwatatulia hayo mengine.
Twawatakia kila la kheri katika kupata suluhisho kwa
Na Allaah Anajua zaidi