Du’aa Hukubaliwa Wakati Wa Kuolewa Au Wakati Mzazi Anapojifungua?
SWALI
Assallam alaykum warahmatu llah wabarakat ama baada ya kumshukuru allah subhanahu wataala na kumtakia rehma mtume Muhammad swalla llah allaih wassalam nina swali nataka kuuliza inshaallah allah atawalipa ujira wenu eti dua ukisoma kipindi mtu anaolewa katika muda ule au kipindi mtu anajifungua huwa ni dua yenye kukubaliwa au uzushi tu.
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu du‘aa wakati wa kuolewa na kujifungua.
Linalofahamika ni kuwa mtu anapooa na siku anakwenda kwa mkewe anatakiwa aweke mkono wake juu ya kichwa cha mke na kusoma du‘aa aliyotufunza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na watu wanafaa wawaombee wanandoa.
Hatujapata kuona Hadiyth yoyote yenye kutaja kukubaliwa kwa du‘aa kwa anayeolewa au anayejifungua.
Na Allaah Anajua zaidi