Mume Ana Tabia Mbaya Alipomkataza Kamtajia Talaka, Naye Ameandika Na Kutamka Talaka, Je Nimeachika?

SWALI:

 

na uliza swali nina wasiwasi nalo kama mume wako hafati mambo ya dini ni mtu mwenye marafiki wabaya wajaribu kukataza atulie hataki kila siku wmakorofishana ukatakaa kuwache pengine itakua dawa atatulia na sio nia yako kuachwa ni hasira na yeye hataki mwisho akaandika talaka bila shahidi kisha akasema sikukuacha ni hasira huwa imepita ama bado ama akikwambia na mdomo nimekuacha huwa imepita maa bado. Asalam aleikum


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu talaka. Tufahamu ndugu zetu kuwa talaka katika Uislamu haina mzaha. Mzaha wake ni ukweli na ukweli wake ni ukweli. Mara nyingi dada zetu hufanya makosa kwa kuwafanya waume zao kutoa talaka kisha baadaye kujuta.

 

Pindi mume anapomwambia mkewe nimekuacha au akaandika kuwa amemtaliki basi talaka huwa imepita hata kama hakuna mashahidi. Kwa hiyo, ikiwa mume ameandika talaka, talaka hiyo inapita hata ikiwa ameitoa kwa hasira. Na ikiwa amesema kwa mdomo pia imepita. Hivyo, tusiifanyie talaka na Dini mzaha.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share