Kutokufanya Waliymah (Karamu Ya Harusi) Kwa Khofu Ya Kuweko Maasi ya Muziki Na Ngoma
SWALI
saalam aleykum,
nilazima kufanya sherehe au kualika watu katika ndoa, je
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Yanayopasa kutendwa katika Nikaah mojawapo ni kutangaza ndoa kwani ni amri kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema:
((أعلنوا هذا النّكاح , واجعلوه في المساجد, واضربوا عليه الدّ فوف))
((Tangazeni ndoa hii, na ifanyeni msikitini, na pigeni dufu)) [At-Tirmidhiy na Ahmad]
Vile vile kufanya Waliymah (Karamu Ya Harusi) ni jambo lilowajibika kwa bwana harusi:
لَمَّا خَطَبَ عَلِي فَاطِمَةُ رَضِيَ الله عَنْهُ قال: قال رَسُولُ الله صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمْ: (( إِنَّهُ لاَ بُدَّ لِلْعرْس مِنْ وَلِيمَة )) وَفِي رِوَايَة ((لِلْعَرُوس))
"'Aliy alipomposa Faatwimah alisema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Hapana budi iwepo karamu, hapana budi bwana harusi afanye karamu)). Msimuliaji amesema: Sa’ad akasema, mimi nitaleta kondoo, na mwingine akajitokeza akasema, mimi nitaleta kadha wa kadha katika mahindi. Katika Riwaaya nyingine ma-Answaar walikusanya mahindi mengi” [Ahmad na At-Twabaraaniy: Isnaad yake inakubalika
Na sio lazima iwe yenye gharama kubwa, chochote kinachopatikana kutokana na hali na uwezo wa bwana harusi.
أَقَامَ النبي صلى الله عليه وسلم بَيْنَ خَيْبَرْ وَالْمَدِينَة ثَلاثَ لَيَالٍ يبني عَلَيْهِ بِصَفِيَّة، فدَعوتُ المسلمينَ إلى وَلِيمَتِهِ، فَمَا كَانَ فِيهَا مِنْ خُبْزٍ وَلاَ لَحْمٍ وما كان فيها إلاّ أن أمرَ بلالاً بالأنطاع فبُسطَت، (وفي رواية) : فَحصت الأَرْض أَفَاحِيص، وَجِيءَ بِالأنْطاَع فَوَضَعت فِيهَا ) ، فَألْقَي عَلَيْهَا التَّمر وَالأَقطْ والسَّمْن [فَشَبَعَ النَّاسُ]
"Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikaa baina ya Khaybar na Al-Madiynah kwa muda wa siku tatu siku ambazo alimuingilia (alimuoa) Swafiyah. Kisha nikawaalika Waislamu katika karamu yake ya ndoa. Hakukuwa na nyama wala mikate katika karamu, bali matandiko ya ngozi yaliletwa na juu yake zikawekwa tende, maziwa makavu na samli iliyo
Kukhofu kwako maasi yasitendeke, inapasa wewe bwana harusi uwe na msimamo wako thabiti na mkali katika jambo hili kwani mwanamue ndiye msimamizi wa mambo baina yake na mke. Hivyo inakupasa uzuie hayo maasi yasitendeke, usiache hayo yakakukosesha kutekeleza yaliyo wajib na Sunnah katika ndoa yako. Jaribu kila njia kuyazuia maasi hayo, na ikiwa umeshindwa kuyakataza, jitahidi kuwapatia Mashekh jamaa zako wanaotaka kutenda maasi katika sherehe ya harusi yako ili uweze kuyazuia
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo kamili yanayohusu kufunga Nikaah na sheria zake.
Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika (Aadabu Az-Zafaaf Fiy As-Sunnat Al-Mutwahharah)
Yanayopasa Na Yasiyopasa Kutendeka Katika Ndoa
Sherehe Za Harusi Ya Kiislamu Yanayohusu Kuimba Na kupiga Dufu
Yanayompasa Bwana Harusi Na Bibi Harusi Siku Ya kufunga Ndoa
Na Allaah Anajua zaidi