Idadi Ngapi Ya Watu Wanaotakiwa Kuwa Mashahidi Wa Jambo Ki Shariy’ah?

 

Idadi Ngapi Ya Watu Wanaotakiwa Kuwa Mashahidi Wa Jambo Ki Shariy’ah?

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Assalaam Alaykum warahmatullaahi wabarakaatu. Mimi ni muislamu, Je ni idadi gani ya mashahidi wanaohitajika kutoa ushahidi juu ya jambo/tukio lolote?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakika mashahidi wanatofautiana kulingana na tukio au jambo lenyewe. Tunakuwekea hapa chini baadhi ya mifano:

 

1. Ikiwa ni suala la uzinzi kunahitajika mashahidi wanne (4) waadilifu.

 

2. Katika kukopeshana kunahitajika mashahidi wawili wanaume, wakikosekana wanaume wawili, basi mwanaume mmoja na wanawake wawili.

 

3.  Katika ndoa vilevile kunahitajika mashahidi wawili.

 

4. Kuanza mwezi mpya katika kalenda ya Kiislamu kunahitajika shahidi mmoja na katika kutoka Ramadhwaan mashahidi wawili kuwa wameuona mwezi. 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share