Nyama Ya Ngamia Na Kasa Halali Kuliwa? Wanyama Gani Tulioharamishiwa Kula Na Nini Sababu Yake?

SWALI LA KWANZA:

 

Samahani kama nitakuwa sikuelewa vema ila ningependa kuhoji hivi?

 

Kuna wakati niliwahi kusikia kuwa kuna makontainer yas nyama ya ngamia yamekuja nchini kwetu kutika Saudi Arabia kwa ajili ya misaada kwa waislam wa tanzania sasa hii inakuwaje au kunamadhehebu ambayo yanahalalisha kula nyama hiyo?

 

kuna wanyama ambao hawarugusiwi kuliwa na waumini wa kiislam ningependa kujua ni wanyama wa aina gani na ni sababu ipi inayo fanya wasiliwe.

 

SWALI LA PILI:

 

Assalaam alaykum warahmatuLLah wabarakatu. Mimi nataka kujua kama nyama ya kasa ni halali au haramu. Maana wapo wasemao halali na wapo wasemao ni haramu kuliwa Kama ni halali naomba ushahidi wa aya au hadith na kama ni haramu ni katika aya ipi na hadithi ipi.


 

JIBU

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uhalali na uharamu wa kula baadhi ya nyama. Hakika ni kuwa nyama ya ngamia na kasa ni halali kuliwa na Waislamu. Ama ngamia zipo Hadithi nyingi za wazi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa wakila, mpaka (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaamrisha mwenye kula nyama hiyo atawadhe (Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah). Ama kuhusu kasa upo msingi wa sheria kuwa vitu vyote ni halali isipokuwa vilivyoharamishwa na sheria na hatujapata Hadiyth kuhusu uharamu wake.

 

Ama nyama ambazo ni haramu vimetajwa kwa ujumla katika Qur-aan. Mfano ni:

 

1.     Nguruwe

2.     Nyamafu

3.     Wanyama wenye kula wanyama wengine au wenye kutumia makucha kuwindia.

 

Hata hivyo, hata kama hatujajua hekima ya kukatazwa vilivyoharamishwa huwa vina madhara kwetu sisi kwani aliyetuekea sheria hiyo ni Mjuzi wa kila kitu na Ndiye Mwenye kujua vilivyo vizuri na vibaya kwetu.

Tafadhali soma jibu lifuatalo upate ufafanuzi zaidi kuhusu swali lako:

 

Wanyama Ambao Tumehalalishiwa Kuwala

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share