Kuku Wakitiwa Maji Ya Moto Kabla Ya Kutolewa Manyoa Hawafai Kuliwa? Na Kuna Hadiyth Inayosema Hivyo?
SWALI:
Assalamu Alaykum WRWB,
Naomba nipewe jibu kwa suala langu hili: Baadhi ya waislamu wanaamini kuwa kuku waliowekwa kwenye maji ya moto kabla ya kutolewa manyoya hawafai kuliwa kwa vile washakuwa haramu. Hujja
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu uharamu wa kula kuku aliyetiwa maji moto akiwa na manyoa yake.
Hatukuweza kuipata Hadiyth hii katika vitabu vya Hadiyth.
Kwa hiyo, kuku baada ya kumchinja unaweza kumtia maji ya moto ili iwe sahali kumtoa manyoa na baadaye kumpika na kumla bila ya tatizo lolote lile, na ni halali wala si haramu kuliwa.
Na Allaah Anajua zaidi