Amemshtaki Mahakamani Akamtisha Atamfanyia Kitendo Kibaya, Naye Akamshtaki, Sasa Miezi Sita Wametengana, Je, Talaka Imeshapita?

SWALI:

 

asalamu alaykum mimi na mume wangu tuna matatizo katika ndoa yetu alikwenda kunishitaki mahakamani na akaniambia atanionesha yaani atanifanyia kitu kibaya mimi aliniogopesha sana kwa maneno yake hayo tulikwenda mahakamani na mimi nikasema hayo maneno aliyoniambia na mahakama ikaamua asiingie ndani ya nyumba yangu kwa sababu ya tamko hilo alilolitamka sasa ni miezi sita sijakutana nae wal hatuzungumzi jee mimi kisheria nimeachika au ninaweza kumdai talaka


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu mume kukutishia kukutenda vibaya.

 

 

Hakika tamko hilo si talaka, kwani talaka kisheria ni lazima itoke kwa tamko la wazi lenye kueleweka kuwa ni hivyo.

 

Hivyo, kujitoa katika utata huo inabidi uitishe kikao baina yako, mumeo na wawakilishi wako na wake. Katika kikao hicho inabidi uelezee yale yaliyotokea kisha uache mume aeleze kama amekutaliki au bado yu mumeo. Ikiwa imeshindikana inabidi uende kwa Qaadhi kama yupo katika sehemu unayoishi na kama hakuna inabidi uende kwa Shaykh aliyewaozesha au Shaykh mwengine yeyote ambaye ni mjuzi wa Dini na muadilifu ili aamue ili upate kupata uhakika na hatima yako kuhusu hilo.

 

Tunakuombea kila la kheri katika juhudi zako kuhusu hilo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share