Hupata Damu Baada Ya Kujimai Na Mume – Vipi Kujitibu Na Majini Wa Mahaba?
SWALI:
Assalam alaykum jamiaan. Bismilah Rahman Rahim,
Nina wingi wa heshima kutoa shukurani zangu kwenu na kwa waislamu wote kwa jumla kwa kutuelimsha na kutueka sawa katika mambo tofauti yanayotupa utata. Mimi ni mwana ndoa, naomba kupatiwa ufumbuzi wa Dua au Visomo vya Ruqya kwa ajili ya kujikinga na majini mahaba ambao wananitatiza sana mimi na mume wangu, mara nyingi huwa natokewa na damu wakati wa kujaamiiiana na mume wangu, nilifika vituo vya afya na kufanya uchunguzi wa njia zangu za uzazi na bahati nzuri alhamdullillah nikaonekana sina tatizo lakini cha kushangaza ni kwamba ikisita damu kama nikiwa mkavu basi sipati raha ya tendo na mume wangu huwa anamaliza mapema sana. Nina mwaka na miezi nane lakini hata siku moja sijaona furaha ya tendo.
Naomba munipe ushauri ili nami nifurahie tendo
Wabillah tawfiq
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako.
Muislamu anatakiwa ajikinge kila wakati kwa kinga ambazo tumeelezewa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ikiwa ni ya Shaytwaani, hasadi na maafa mengine yanayotokana na hayo.
Kinga inatakiwa ichukuliwe kabla ya kukumbwa na janga
Jambo la kwanza ni kuanza kusoma Aayah au Surah za Qur-aan zinazohusiana na suala
Kusoma Aayah kumi za al-Baqarah (2) ambazo zinaepusha nyumba zetu na Mashaytwaan. Nazo ni kuanzia Ayah 1-5, 255-257 na 284-286. Hizi Aayah zinatakiwa zisomwe asubuhi na jioni.
Kusoma Suratul Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas mara tatu tatu, asubuhi na jioni na pia wakati wa kulala.
Na Qur-aan yote ni dawa inatakiwa kila Muislamu awe na ada ya kuisoma na kujua maana yake na kutekeleza yaliyomo ndani yake.
Usome du’aa ambazo ni kinga unapotoka nyumbani na unapoingia.
Du’aa ambayo wewe na mumeo mnatakiwa msome wakati wa kitendo cha ndoa ambayo inawalinda na kukilinda kitoto kitakachoingia na Shaytwaan.
Adhkaar za baada ya Swalah na pia wakati wa kulala.
Usome adhkaar za asubuhi na jioni.
Adhkaar nyingine ni
Na hizi adhkaar pamoja na nyingine unaweza kuzipata katika kijitabu ambacho ni muhimu
Pia bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi yam as-ala haya:
Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao
Anapoweweseka Usiku Asomewe Surah Gani?
Nimeambiwa Nina Jini La Kiislamu Kwa Sababu Ya Kupenda Sana Dini
Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi
Jambo la pili, ni wewe na mume wako kwenda kwa Shaykh aliye mjuzi wa mas-ala ya Ruqyah ya kisheria, ambaye ni mchaji Mungu aweze kuwasomea kwa njia ya Kishari’ah na InshaAllaah mtapona na ugonjwa wenu huo.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awapatie shifaa ya haraka.
Na Allaah Anajua zaidi