Kazi Isiyokuwa Na Likizo Za Siku Za Dini Ya Kiislaam Na Hawezi Kuswali Swalaah Ya Dhwuhaa

SWALI:

 

assalam alaykum warrahmatullah wabarakatuh.

Mimi nauliza jee huu ni uislamu au nikutafuta utajiri au ni njia za sheitani.

Mimi nimeajiriwa katika taasisi fulani lakini katika taasisi hiyo bosi ameniambia hakuna j'pili sawa hakuna j'mosi sawa hakuna public holidays sawa lakini pia hata religion holidays pia hakuna tunakwenda kazini mpaka saa saba na kabla ya kazi nilikuwa napata kuswali: swala ya dhuha kwa wasaa lakini tokea nimeajiriwa katika kazi hii sasa ni mwezi wa tatu sijaswali hii ni sawa? Naomba jibu.

 


 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutopata wasaa wa kuswali ukiwa kazini.

 

 

Ndugu yetu tufahamu kuwa kazi ni ‘Ibaadah kama vile Swalah na ‘Ibaadah nyingine kila moja kwa daraja yake. Kwa ajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Akatutaka tuombe kwa kusema:

 

 

Na katika wao wapo wanaosema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto!” (Al-Baqarah [2]: 201). Na Akaufanya Aliyetukuka mchana ili tupate kupata maisha yetu kwa kufanya kazi:

Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?” (an-Nabaa’ [78]: 11).

 

Kwa kawaida, kazi ni mapatano baina ya mwajiri na mwajiriwa. Hivyo, ni muhimu kabla ya mtu kukubali atazame mkataba baina yao asije akajuta. Ama kufanya kazi siku ya Jumamosi, Jumapili na hata Ijumaa yenyewe au siku kuu haikatazwi kishari’ah. Pia ni muhimu kwa Muislamu kushikama na ‘Ibaadah ya Sunnah kwa jinsi anavyoweza. Na suala la kuswali dhuhaa halina utata wala halitochukua muda mwingi. Hatujui mazingira ya hapo ulipo lakini katika kazi nyingi huwa kuna mapumziko ambayo watu wanakunywa chai, wewe unaweza kutumia fursa hiyo kwa kuswali Swalah ya dhuhaa. Ikiwa hakuna kipindi hicho unaweza kuzungumza na bosi wako ili akupe dakika tano ya kuweza kuswali Swalah hiyo ukiwa ofisini kwako au sehemu yako ya kazi.

 

Tunakuombea kila la kheri.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share