Mume Anataka Kuridhishwa Na Mkewe Kwa Kutumia Mkono Wakati wa Hedhi Au Nifasi

Assalam aleikum warahmatuAllah wabarakatu swala langu ni juu ya mume wangu hupendelea nitumiye mkono wangu kiswahili ni ngumu kwangu kuandika nitatumiya kiengereza my husband prefers me to use my hand to make him come (sexual satisfaction using my hands even when I am available for him to use for his pleasure) when I am in nifaas or even in my periods is it allowed for me to do that? When I tell him I am not sure about this he quotes the aya in sura al baqarah nissaukum harthum lakum fautuu harthakum annashi’tum please advise me.

 

 


 

 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mume kutaka kuridhishwa na mkewe kwa kutumia mkono.

 

Kwa hakika utumiaji wa mkono ni katika vitangulizi vya kujitayarisha kwa jimai yenyewe. Na Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo” (al-Baqarah [2]: 223).

 

Na Allaah Aliyetukuka Amesema tena:

Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watwaharike. Wakisha twahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Allaah” (al-Baqarah [2]: 222).

 

Na kuhusu hizi Aayah zipo Hadiyth nyingi sahihi zinazotujulisha kuwa mwanamke akiwa katika hedhi au nifasi, mume anaweza kustarehe naye anavyotaka isipokuwa kumuingilia kwa nyuma au kujimai naye. Kumuingilia mwanamke nyuma ni haramu japo kuna wanaojiita Waislamu wanahalalisha hilo wake zao wanapokuwa katika hedhi!

 

Hivyo, mke atafunga kitambara sehemu ya uchi wake na mume atastarehe naye vile anavyotaka isipokuwa kufanya naye hayo mambo mawili.

 

 

Mafunzo haya tunapata katika masimulizi yafuatayo:

 

 

Ya kwanza:

 

 

 

((...اصْنَعُوا كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ))

 

"…fanyeni kila kitu isipokuwa jimai pekee"  [Muslim, Abu 'Awwaanah na Abu Daawuud]





Ya Pili:

 

عن عَائِشَةَ رضي الله عنها ، قَالَتْ:  كانَ رَسُولُ اللَّهِ، يَأْمُرُ إِحْدَانَا إِذا كَانَتْ حَائِضاً أَنْ تَتَّزِرََ ثُمَّ يُضَاجِعُهَا زَوْجُهَا وَقالَتْ مَرَّةً: يُبَاشِرُهَا.

Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Tulipokuwa katika siku zetu (hedhi) Mtume alikuwa akituamrisha tuvae nguo kiunoni ili mume aweze kulala naye". Na akasema (mama wa waumini ‘Aaishah) pia …"Mumewe aweze kumkumbatia na kumpapasa" [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 


Ya Tatu:

عن بَعْضِ أزْوَاجِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قالَتْ: إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إذَا أرَادَ مِنَ الْحَائِضِ شَيْئاً ألْقَى عَلَى فَرْجِهَا ثَوْباً [ ثم صنع ما أراد]  

Kutoka kwa mmoja wa wake zake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipokuwa anataka kitu (kufurahi naye) kutoka kwa wake zake siku za hedhi, alikuwa anaweka nguo katika sehemu zake za siri kisha hufanya anavyotaka" [Abu Daawuud: Swahiyh]

 Pia bonyeza kiungo kifutacho:

 

16 Makatazo Ya Jimai (Kitendo Cha Ndoa) Wakati Wa Hedhi

 

  

Kwa hiyo, hakuna tatizo lolote kwa mke kumstarehesha mume wake kwa njia hiyo. Hata hivyo kuna wanachuoni wanaoona kuwa, anaweza mke kumchezea mumewe kwa mkono ila tu isiwe ni kama anavyofanya jimai. Inatakiwa iwe ni kuamsha hisia tu sio kumaliza hisia za jimai, kwani kutekeleza hilo kila mara litamfanya mume aue maume yake na kushindwa kumstarehesha mkewe mbeleni. Na hilo laweza kuleta matatizo mengi katika uanandoa wenu.

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share