Kutokufanya Tendo La Ndoa Kwa Muda Mrefu Kunaleta Madhara?
SWALI:
Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh,
Nawashukuru kwa website yenu kwani anatuelisha
Swali.Mimi nimsichana wa umri wa miaka 23 na mpaka hivi sasa sijawahi kufanya tendo la ndoa, kwa sasa nimebahatika kupata mchumba lkn kwakweli namshukuru Allah kwani hajawahi hata kunitamkia jambo hilo na nimekuwa na ye
kwa muda mrefu,je ikiwa hujafanya tendo hilo kwa muda mrefu huleta madhara?kwani nimepata tetesi kuwa ikiwa hujafanya jambo hilo kwa muda huleta madhara ya kisaikolojia.
Nitashukuru nikipata ufumbuzi wenye uhakika juu ya jambo hili kwani nashindwa kwa kuwa si jambo jema mbele ya Allah.
Wabillah tawfiq
JIBU:
AlhamduliLLah, Waswalaatu Was-salaam 'alaa Rasuli-Llah صلى الله عليه وآله وسلم Amma ba'ad,
}}وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ{{
((Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila
[Al-Baqarah : 120]
Allaah سبحانه وتعالى Ametuhimiza kuingia katika ndoa
((Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu Atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua))
An-Nuur:32
Vile vile Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema kuwa kufunga ndoa ni kukamilisha nusu ya dini yake Muislamu
روى أنس بن مالك رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وأله وسلم قال ((إذا تزوج العبد ، فقد اسـتكمل نصف الدين فليتق الله فيما بقي )) رواه الطبراني وحسنه الألبان
Imetoka kwa Anas bin Maalik رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Atakapofunga ndoa mja, huwa amekamilisha nusu ya dini, basi amche Mwenyeezi Mungu kwa nusu iliyobaki ))
[At-Twabaraaniy, na Sheikh Albaaniy amesema ni Hasan]
Muislamu anatakiwa kutimiza Sunnah hii ya kufunga ndoa bila ya kuchelewa kuepukana na madhara mingi. Kwa hiyo ndugu yetu tunakupa nasaha muhimu yenye manufaa kuwa ingia katika ndoa na huyo mchumba madam ni Muislamu na hatuoni kuwa umetaja sababu yoyote ya kukuzuia kufunga naye ndoa.
Na ikiwa hukuweza kufunga ndoa kwa muda wowote kwa sababu fulani basi inakupasa ujihifadhi na kujiweka katika heshima na stara hadi utakapojaaliwa kufunga ndoa
((وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّى يُغْنِيَهُمْ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ .. ))
((Na wajizuilie na machafu wale wasiopata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu Awatajirishe kwa fadhila yake))
[An-Nuur: 33]
Kuchelewa kuolewa haina maana kwamba itakuletea madhara ya kisaikolojia ikiwa utabakia katika Twa'a ya Allaah سبحانه وتعالى , kwani hayo ni katika majaaliwa ya Allaah سبحانه وتعالى na muumini anatakiwa akubali na kuridhika majaaliwa yote.
Na hizi habari za kupata madhara ya kisaikolojia, zimeletwa na Makafiri wanaotaka kuwatoa waislam katika maadili
Na ndio maana Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliamrisha kuwa ni bora kufunga kwa yule ambaye hakuweza kufunga ndoa ili kuepukana na hatari ya maasi
))يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ مَنْ اسْتَطَاعَ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ(( البخاري ومسلم
((Enyi vijana, anayeweza kuoa basi na aowe kwani ni lindo la macho (na kutazama ya kutamanisha) na ni hifadhi ya tupu (kwa kufanya zinaa) Na asiyeweza basi afunge (Swawm) kwani ni kinga (ya matamanio) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Wa Allaahu A'alam.