Anapokuwa Safarini Mke Wa Pili Hataki Kuwasiliana Naye, Na, Anamjibu Ujeuri, Je, Amuache Kwa Tabia Yake Hiyo?
SWALI:
A.w.w. Mimi na wake 2. Napokua safarini
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mke kuwa mjeuri kwako.
Matatizo na shida za kuoa mke mmoja au wawili zinatokea kwa mume kufanya uchaguzi mbaya kwa mwendani wake katika maisha yake.
Hata hivyo, kukitokea tatizo au matatizo ya kindoa hutakiwi wewe
“Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Allaah Ametia kheri nyingi ndani yake” (an-Nisaa [4]: 19).
Unaweza kufanya yafuatayo kabla ya kuchukua hatua yoyote ile.
1. Huenda kuwa mke wako hajui wajibu wake kwako. Kwa hivyo, fanya juhudi umpeleke katika Madrasah ya sawa ili aweze kupata mafunzo ya Dini yamwezeshe kuishi Kiislamu.
2. Jaribu kuzungumza naye kuhusu mas-ala ya kidini kwa kumletea vitabu vya Dini, VCD, DVD, CD na kaseti za mawaidha kuhusu maudhui tofauti za Kiislamu (Nyingi zipo tayari ALHIDAAYA hapa Mawaidha, Swahili Video). Unaweza kutumia watu wake wa karibu ili wazungumze naye. Mas-ala ya kushauriana ni muhimu
3. Ikiwa hajajirekebisha basi itabidi uitishe mkutano baina yako wewe, mkeo, wazazi wake na wazazi wako. Wakikosekana, unaweza kuwaita wazee wengine wazoefu katika mas-ala ya upatanishi na wenye kutaka maslahi ya ndoa kubakia.
4. Ikiwa hadi hapo hamkupata suluhu ya mkeo kujirekebisha basi itabidi mwende kwa Qaadhi ili aweze kuwapatanisha au kwa Shaykh mzoefu, mcha Mngu, mwenye elimu na muadilifu ili awasikilize.
Hata hivyo, kw aupande mwengine huenda ikawa kosa ni lako. Na lau kadhiya hiyo tutakuwa tumeielewa vyema basi utatuondoshea utata wowote ule.
Tulivyoelewa ni kuwa mke/wake zako wanaishi nyumba mbali mbali ila tu wakati unasafiri unamchukua mke mdogo unampeleka kwaenye nyumba ya mke mkubwa.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Mke Mjeuri Juu Ya Kwamba Anapewa Raha Na Mahitajio Yote Na Mume
Mke Mjeuri Sana - Anamwambia Mtoto Wangu Kuwa Nimeshakufa, Nifanye Nini?
Twakutakia kila la kheri na kutatua tatizo
Na Allaah Anajua zaidi