Zawaaj (Ndoa) Ya Al-Misysaar - Nini Hukmu Yake?
SWALI
Assalam alaykum warahmatu llahi wabarakatuhu,
Tafadhali ningeomba kutoka kwa masheikh wetu wa al hidaaya, nifafanuliwe nini maana ya "zawaj misyar".
Nilivyo fahamishwa ni hivi:
Ni ndoa ambayo haina mambo mengi
Jee hii ndoa inakubalika kisheria kiislamu. Wassalam alaykum warahmatu llahi wabarakatuhu.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ndoa ya Misyaar.
Zawaaj al-Misyaar (ni aina ya ndoa) ambayo inagawanyika sehemu mbili. Nazo ni
1) Zawaaj al-Misyaar inamaanisha kufungwa ndoa baina ya mume na mke. Mkataba unatimiza masharti yote ya ndoa ya kawaida
2) Aina ya pili ya Zawaaj al-Misyaar ni mkataba ambapo ana jukumu la kumkimu mkewe kifedha, hata hivyo, hatompatia mgao wa sawa kuhusiana na kulala kwake kwa zamu. Aina hii ya Zawaaj al-Misyaar ndio iliyo maarufu zaidi kwa kuwa mume anataka kuiweka ndoa yake kuwa siri ili mkewe asiwe ni mwenye kujua lakini inatimiza mahitaji yote ya ndoa ya kawaida.
Ama kuhusu aina ya kwanza ya Zawaaj al-Misyaar, tunafikiria kuwa ni matakwa ya mwanamke kutaka kujihifadhi na zinaa na pia kuwa na Niyah ya kupata mtoto au watoto ambako kunampelekea katika ndoa hii. Hivyo, aina zote mbili zinakubalika na ni halali. Ama kule kukubali kuacha baadhi ya haki ya mmoja wa wakeze mume katika ndoa aina hii haina utata wowote maadamu tafanywa kwa ridhaa na kutakuwa na maslahi kabla au baada ya mkataba wa ndoa hiyo.
Hakika, Zawaaj al-Misyaar inawapatia wanandoa baadhi ya faida
Na ndoa hii haiwezi kabisa kufananishwa na ndoa ya muda ‘Mut’ah’ ambayo wanaiofanya Mashia yenye kukosa masharti ya ndoa na yenye malengo ya kujistarehesha kimwili tu. Na wale wanaotyaka kufananisha baina ya Misyaar na Mut’ah, lengo lao ni kutafuta sababu penginepo ili kuhalalisha makosa
Na Allaah Anajua zaidi