Amekhasimikiana Na Mumewe Muda Wa Miaka 15 Mume Hamuulizi Lolote Na Hakumtamkia Kuwa Kamuacha, Je Ameachika?
SWALI:
ASALAAM ALYEKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU. KWANZA NAWAPONGEZA KWA KAZI NZURI MNAYOIFANYA.SWALI LANGU NDUGU YANGU TOKA AOLEWE ANA MUDA WA MIAKA 20 AMEISHI NA MUME WAKE MIAKA 6 WAKAASIANA MUME WAKE AKAENDA KUOA .HAMUULIZIA KWA LOLOTE.KWA MUDA WA MIAKA 15 HIYO.JE ATAKUWA AMEACHIKA JAPO HAJAWAHI KUMWAMBIA NIMEKUACHA.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mke kukhasimiana na mumewe kwa muda wa miaka 15.
Hakika kila Dini ina nidhamu yake katika kila jambo na kwa kuwa Uislamu ni nidhamu kamili ya maisha kuhusu kila jambo, ikiwemo mas-ala ya talaka.
Tujue kuwa talaka Kiislamu inapita tu ikiwa mume atatamka kuwa amemtaliki mkewe, au amemwandikia barua kuhusu suala
Katika hali hiyo dada yetu ilikuwa ampigie simu mumewe au akutane naye kujua hatima yake katika kuachwa huko. Kwa kuwa hakufanya hivyo, itabidi kwa sasa awe ni mwenye kufuatilia suala
1. Je, mke bado anataka kubaki na mume huyo? Ikiwa atataka hivyo atakuwa na haki hiyo bila ya pingamizi yoyote. Hata hivyo, inatakiwa ahakikishe kuwa atapata haki yake kikamilifu kama inavyohitajika kutoka kwa mumewe
2. Mume hakujibu chochote hata baada ya kupigiwa simu au kuendewa, itabidi mke afanye juhudi aitishe kikao baina yake na mumewe na wazazi au wawakilishi wao ili wasuluhishe tatizo
3. Ikiwa hakukupatikana suluhisho lolote itabidi mke apeleke kesi yake kwa Qaadhi au Shaykh muadilifu, aliye mjuzi ili kuamua tatizo
Hata hivyo, nasaha zetu hasa kwa kina mama ambao wamedhulumiwa wasiwe ni wenye kudhalilishwa kwa muda mrefu
Na Allaah Anajua zaidi