Ami (Baba Mdogo) Anaweza Kuwa Walii Japokuwa Baba Mzazi Yupo Na Ametoa Idhini?

 

SWALI

 

Je, Baba mdogo anayoruhusa ya kuwa walii kama baba mzazi wa mtoto yupo ila ameidhinisha iwe hivyo?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ami kuwa walii wa mtoto. Ami kisheria hawezi kuwa walii ikiwa baba mzazi yupo. Hata hivyo, ikiwa baba mzazi amemuwakilisha ndugu kuwa ndiye awe anatoa idhini ya binti zake basi uwakala huo wa uwalii unakuwa sawa.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share