Sina Utulivu Katika Ndoa Yangu Baada Ya Kudanganywa na Mume Wangu Pamoja na Mama Mkwe
SWALI:
MIMI NIMEOLEWA MIAKA MIWILI. SINA UTULIVU KABISA KATIKA NDOA YANGU. BAADA YA SIKU MBILI YA HARUSI MUME WANGU ALIKUWA NA KAMA WASIWASI, HASA WAKATI WA 'KULALA' ALINISIMULIA KUWA KUNA MSICHANA WA UKOO WAO AMBAE WATU WAKE HUYO MKE WALIMTAKA AMUOE, LAKINI YEYE HAKUMTAKA WALA MAMAKE PIA. AKAHOFIA PENGINE WAMEMFANYIA KITU. NILIGUNDUA JAMAA ZAKE HAWANA FURAHA WANAPONIONA MIMI MPAKA SASA. ALIAMBIWA MAMANGU NA MWANAMKE AMBAE NI JAMAA YA MUME WANGU KINYUME YA MANENO AMBAYO YALINICHOMA
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mahusiano yako na mumeo. Mwanzo dada yetu tunakushauri
Utulivu hauji tu hivi hivi. Bali watu wengine wasio wapendelea wenziwao mema hujaribu kila njia kuleta bughudha na kutosikilizana baina ya watu wawili wapendao au wenye mafungamano ya
Mume wako kukusimulia yaliyopita ni jambo zuri kwani ungekuja jua hayo baadaye ungehisi kuwa mumeo amekuficha na hivyo hakukutakia kheri. Mumeo aliona kuwa ana pili wake ambaye angeweza kumtegemea katika matatizo ya kimaisha anayo kumbana nayo ili muweze kusaidiana. Na lengo la ndoa ni hivyo muweze kusaidiana ili kukabiliana na changa moto zozote zile na matatizo. Dunia ni mitihani na kila mmoja wetu atafikiwa na mitihani ya aina yake yaliyo tofauti na mwenziwe. Leo ni mumeo ana dhiki na shida kesho inaweza kuwa ni wewe au mmoja wa familia yako. Wakati huo utahitajia mumeo asimame na wewe kwa kukushauri, kukuliwaza na kukupatia moyo au akwambie shauri yako, hayo niko sio yangu.
Hakika ni kuwa jamaa zake hawawezi kuwa na furaha na mumeo kwani waliona atamuoa binti
Tunakupongeza kuwa nawe ulikuwa mkweli kwa mume wako kwa kumwambia uliyoyasikia kwa lengo la kutaka kujua ukweli na kutatua tatizo
Isitoshe mama mkwe wako amekuelezea pamoja na kuapa kuwa hayo uliyoelezwa sio ya kweli, hata hivyo wewe bado hujatosheka, hujaridhika wala kuamini. Huu ni mtihani kwako na pia kwa mumeo hivyo unatakiwa kuwa na subira na uongoze Ibaadah na bila shaka Allaah Aliyetukuka Atakusaidia kwa njia muruwa kabisa. Usichukie nafsi yako bali jitahidi kufanya mema na jirekebishe na njia yako itakuwa nzuri hapa duniani na Kesho Akhera.
Na Allaah Anajua zaidi.