Katembea Na Mume Wa Rafiki Yake, Kaomba Msamaha
SWALI:
Salaam aleykum, nimelala na mme wa mtu nikaona vibaya nikaomba samahani kwa mkewe akanisamehe yakaisha, baadae mme wa yule dada akanifata tena na mimi na mapenzi nae tukaendelea kufanya hivyo vitendo tena sio mara moja nimemwambia tuoane anababaisha lakini kuzini na mimi ndo kazi yake, ni aibu wala sioni sifa kwa sababu namuogopa mwenyezi mungu nasali sala tano ila hapo tu kwenye zinaa na huyo mme wa mtu ndo nashindwa ila Alhamdulillah nimeamua kuacha sema tatizo lipo hapa natamani kumuomba mkewe samahani lakini nashindwa kwa sababu mwanzo aliumia sasa wenyewe wanapatana naogopa kuwagombanisha tena sielewi tamuomba vp samahani, NIMEPATA MCHUMBA NAOGOPA ASIJE AKAONA NAMUACHISHA YY ME LABDA TAOLEWA, nifanyeje? Nijibu haraka jamani nipo kwenye wakati mgumu sitaki kuolewa bila kumuomba samahani nikisubiri je huyo atakaekua mume wangu akisikia, naombeni ushauri jamani.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutembea na mume wa mtu.
Hakika ni kuwa zinaa ni katika madhambi makubwa ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameliwekea adhabu kali
Kazi ya Swalah ni kukuzuilia wewe ‘Faahishah’ ambayo ni zinaa na maovu yote. Vipi utakuwa unaswali kisha unatembea na mume wa watu na unazini naye.
Kama Muislamu, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatulezea kuwa,
“Muislamu haumwi na nyoka kwenye tundu moja mara mbili”. Itakuaje wewe uwe utazini mara ya kwanza na usamehewe mbali na kuwa jambo
Tufahamu kuwa masharti ya kukubaliwa toba ni manne inapoingia haki ya mwanadamu katika suala lako
1. Kujiondoa katika maasiya.
2. Kujuta kwa kufanya dhambi
3. Kuazimia kutorudia tena kosa
4. Kuomba msamaha kwa uliyemkosea.
Katika kosa
Ufahamu kuwa malipo mara nyingine ni hapahapa ulimwenguni,
Ushauri wetu nenda tena ukaombe msamaha kwa mke wa mume kama inawezekana na hakutotokea madhara yoyote yale kwa kufanya hivyo, basi ni bora kufanya. Lakini ukiwa atahofia kutokea matatizo au shari kwa kufanya hivyo, ni bora uepuke na uombe Istighfaar sana na umuombee du'aa njema huyo aliyemfanyia ubaya na kumfanyia wema ukiweza.
Na Allaah Anajua zaidi