Tumtii Mama Mshirikina Na Kuishi Naye?
Tumtii Mama Mshirikina Na Kuishi Naye?
SWALI:
Asalam aleykum,
nashukuru kwa majibu yenu. ila nina swali linalonisumbuwa sana kwa kweli ni mtihani, katika familiya yetu tumezaliwa 9. kwa mama yangu tuko 6, na kwa mama wa pili ni 3.waliachana toka mwaka 2007, kwa matatizo tu, na kukosa kuwaminiana .tukaendelea kuishi na baba yetu mzazi akaowa, mwaka 2007/10 baba yetu akaaga dunia, tukabaki na mama yetu wa kufikia na wote tukamuwa tuake wote pamoja mama mzazi wetu toka wachane alirudi kwao. alivyo fariki baba mama akataka watoto wake twende tukakae naye, wa mama tupo wasichana wa nne, wa vulana wawili moja wa kike ameolewa, yuko kwake kwa mumewe. ila tuliyobaki wote tuko pamoja. wa kiume aliyo kuwa mkubwa ndiyo msimamizi wa familiya.
Tatizo ni kwamba mama na baba waliwahi kugombana kwa ajili ya mali kati yao.na pia mama alikuwa anatabiya ya shirki. swali langu ni, mama yangu anataka tuwende tukakai naye tuwache hawa mayatima yani wadogo zetu na mamayao peke yao. na ukitazama hawa ngugu yoyote karibu. kaka yangu akamuliza mama je uanuhakika gani kama utaishi maisha mile hapa duniani?. hana la kujibu, kwakweli ni mtihani sasa analolifanya ni shirki na mpaka sasa hivi anatuma jini na mambo kibao, inavyosemekana kwamba anaagizisha majinina ndiyo kazi yake.
swali langu ni hivi tkimlea na kumti ila awe mbali na sisi kwa sababu tukikanaye atatufarakisha hata sijui tufanyeje kwa kweli tunataka dua ya ke ila ni mtiha tafadhali kwania ba ya ndugu zangu wote naomba utujibu swali hii tufanyeje?
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Uislamu umempa haki mama ya kumfanyia wema hata kama si Muislamu. Kwa maana kuwa kama mama wa mtu ni mshirikina au kafiri basi huyo ni mama yake na hatokuwa na mama mwengine hapa duniani. Hivyo basi, Uislamu unamtaka amfanyie wema bila ya kusahau haki ya Rabb wake na wakati wowote ule atakapokutaka huyo mama kwenda kinyume na maamrisho ya Allaah hutotakiwa kumtii wala kumsikiliza; Allaah Anasema:
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾
Na Tumemuusia insani kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka mwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako; Kwangu ndio mahali pa kuishia. Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Na suhubiana nao kwa wema duniani, na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu. Kisha Kwangu ndio marejeo yenu, na Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. [Luqmaan: 14-15 ]
Jitahidi pia mumlinganie, na kama hamna elimu ya kufanya hivyo, mtafutieni vitabu au mawaidha yenye kuelezea ubaya wa ushirikina na mas-ala ya uchawi. Pia mnaweza mkamtafuta mwenye elimu hapo mlipo na akajaribu kuzungumza naye na kumuaidhi huyo mama yenu. Bila kuacha kumuomba sana Allaah katika Swaalah zenu Awaondolee matatizo hayo na Awatengenezee familia yenu iwe katika utiifu kwa Allaah na kuwa mbali na maovu ya ushirikina na uchawi.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:
Wazazi Wangu Wako Kwenye Maasi,Ushirikina Wa Waganga Na Albadiri (Ahlul-Badr)
Mke Wangu Na Mamake Wachawi Siwezi Kumwambia Dhahiri
Mwanamke Mchawi Anatekeleza Sana Ibada Lakini Anafanya Uchawi Wa Kuua Watu, Vipi Ibada Zake?
Na Allaah Anajua zaidi