Ikifika Wakati Wa Magharibi Anaona Dhiki – Asome Du’aa Gani Kuondosha Dhiki?

SWALI:

 

 

 

Asalam aleikum natumai hapo mulipo nyote hamuna neno.mimi nina swali huwanasikiya dhiki sana  wakati wa magharib  ,hata sijui nini kwanini najaribu kumlani shetwani .sasa naomba munisaidiye na dua ipi ambayo nitaisoma iniodoshe hiyo dhiki na wasi wasi.naomba usaidizi wenu

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tunasikitika kufikwa na hali hiyo, na yakufanya ili kuepukana na hali hiyo ni yafuatayo:

 

  1. Kusoma Qur-aan kwa wingi
  2. Kumdhukuru Allaah Subhaana wa Ta’ala kila mara
  3. Kusikiliza mawaidha
  4. Kudumisha kusoma nyiradi za Asubuhi na jioni kwa mfululizo kwani zinafaika kubwa ya kuondosha kila dhiki, shari na balaa na kumbakisha Muislamu katika usalama, amani na furaha.

Bonyeza viungo vifuatavyo:

 

 

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

028-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Kulala

 

029-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapojigeuzageuza Usingizini Usiku

 

030-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Wasiwasi Usingizini Au Kusikia Uoga Na Mfadhaiko

 

031-Hiswnul-Muslim: Ipasavyo Kufanya Na Kusema Mwenye Kuota Ndoto Njema Au Mbaya

 

034-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ukiwa Na Wahka Na Huzuni

 

 

035-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapopatwa Janga Au Balaa

 

 

128-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuzuia Vitimbi Vya Mashaytwaan

 

 

Pia:

 

Du’aa Za Ruqyah (Kinga) Faida Na Sharh Zake

 

Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah

 

Tafadhali bonyeza pia kiungo kifuaacho upate manuafa zaidi:

 

Nina Dhiki Na Nina Woga Sana Nifanyeje?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share