Vipi Kutofautisha Hadiyth Sahihi Na Dhaifu?

SWALI:

 

 

A.a nivipi kuthibitisha hadith dhaif na hadith swahih?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kutofautisha baina ya Hadiyth Swahiyh na zile ambazo ni dhaifu.

 

Hii ni fani katika somo la Sayansi ya Hadiyth, somo ambalo lachukuliwa kwa muda usiopungua miaka minne kwa mwanafunzi ili kupata shahada ya kwanza.

 

 

Ama Hadiyth iliyo Swahiyh huwa na sifa zifuatazo:

 

1.     Isiwe inapingana na Aayah ya wazi ya Qur-aan.

 

 

2.     Ni lazima itaje kwa uwazi kabisa kuwa kitu kadhaa kilisemwa au kufanywa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

3.     Mpokezi ni lazima awe shahidi kwa tukio analolisimulia.

 

 

4.     Ni lazima itolewe ushuhuda kuwa kila mpokezi alikutana na yule kabla yake katika Isnadi.

 

 

5.     Kila mpokezi katika Isnadi ni lazima awe ni mtu anayejulikana kwa uchaji Mungu, uaminifu, ukweli na utendaji wa ‘amali nzuri.

 

 

6.     Kila mpokezi katika Isnadi ni lazima awe anajulikana kwa kisomo na akili muruwa, na muweza wa kufahamu barabara na kuyafikisha kwa uaminifu na uhakika kwa wengineo yale aliyoyasikia.

 

 

7.     Ni lazima ithubutu kuwa wapokezi wote walikuwa katika zama ambazo walikuwa na uwezo wa kuyafahamu vilivyo yote waliyoyasikia.

 

 

 

Ama kinyume na hizo sifa inafanya Hadiyth kuwa dhaifu, munkar au iliyozuliwa.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:

 

 

 

Maana Ya Hadiyth Dhwa'iyf

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share