Du'aa Ya Kunywa Maziwa
Ipi Ni Du’aa Ya Kunywa Maziwa?
SWALI:
Which dua was (the Prophet) saying before drinking milk. Only Milk not other drinks like water or juices. Please advise.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Mafunzo ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kuhusu chakula au kinywaji ni kama ifuatavyo:
عن عبد الله بن عباس رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه و سلم أنه قال: ((من أطعمه الله طعامًا، فليقل: اللهم بارك لنا فيه، وأطعمنا خيرًا منه، ومن سقاه الله لبنًا فليقل: اللهم بارك لنا فيه، وزدنا منه، فإنه ليس شيء يجزئ من الطعام والشراب غير اللبن)) رواه أحمد وأبو داودو قال الألبان حديث حسن
Imetoka kwa Abdullahi Bin 'Abaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Atakayelishwa chakula kutoka kwa Allaah aseme "Ee Rabb Tubarikie nacho, na Utulishe (chakula) bora kuliko hiki"; Na atakayenyeshwa Maziwa na Allaah aseme, Ee Rabb Tubarikie nayo, na Tuzidishie" kwani hakuna kitu kinachojazilia katika chakula na kinywaji isipokuwa Maziwa)) [Ahmad, Abuu Daawuwd, na kasema Imaam Al-Albaaniy ni Hadiyth Hasan]
Kwa hiyo duaa ya kunywa maziwa ni kusoma du’aa ifuatayo:
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا فيهِ وَزِدْنا مِنْهُ
Allaahumma Baarik lanaa fiyhi wa Zidnaa minhu
“Ee Allaah Tubarikie kinywaji hichi na utuzidishie”
Na Allaah Anajua zaidi