Ulikuwaje Ukataji Nywele Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)?

 

SWALI:

 

How was he (The Prophet (s.a.w.) cutting his hair.  Please advise also,

 

 


 

 

JIBU:

 

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kutokana na hadiyth ifuatayo hapa chini tunapata mafundisho kuwa hivi ndivyo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  alivyokuwa akitaka nywele zikatwe na pia tunaona makatazo ya aina za ukataji nywele vilevile katika hadiyth hiyo:

((Imetoka kwa 'Ubaydullah bin Hafs, kwamba 'Umar bin Naafi'i kamwambia kwamba Naafi'i Mawla 'Abdullah alimsikia 'Umar akisema: "Nimemsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  akikataza Al-Qaza". 'Ubaydullah akaongeza kusema: "Nikauliza; Nini Al-Qaza?"  'Ubaydullah akaonyesha (ishara ya kichwa chake) kutuonyesha sisi na akasema;  Naafi'i kasema, "ni wakati mvulana anaponyoa nywele zake anapoacha kishungi cha nywele hapa na kishungi cha nywele pale". 'Ubaydullah akaashiria mbele ya kichwa (karibu na kipaji) na pembeni mwa kichwa chake. 'Ubaydullah akaulizwa; "Je, hii pia inawahusu wote wasichana na wavulana?"  Akasema, "sijui   lakini Naafi'i kasema, mvulana". 'Ubaydullah akasema, "nilimuuliza Naafi'i tena na akasema, kuacha nywele mbele ya kichwa karibu na kipaji cha uso na nyuma ya kichwa cha mvulana, sio haraam, lakini Al-Qaza ni kuwacha shungi la nywele mbele ya kichwa bila ya kunyoa wakati hakuna tena nywele upande mwengine wowote wa kichwa na kuacha baadhi ya nywele katika pande za kichwa"))  (Al-Bukhari).

Hadiyth hii sahihi inaonyesha wazi jinsi inavyotakikana Muislam kunyoa nywele zake, yaani anyoe usawa mmoja kichwa kizima kwa kiasi anachotaka bila kuzidisha upande mmoja na kupunguza upande mwingine, au kumaliza sehemu za chini na pembeni mwa kichwa na kuacha sehemu ya juu ya kichwa kwa namna inavyojulikana kwa jina la 'panki' katika zama hizi. Hayo ni matendo ya kuwaiga wasio waislam kama wanamuziki, wachezaji mpira au wacheza sinema ambao kwa masikitiko makubwa leo hii ndio wamekuwa kigezo 'good example' cha wengi wetu, tumemwacha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  kuwa kigezo chetu na kuwafuata hao wasiotunufaisha na umaarufu wao wala pesa zao!!   

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share