Kunyoa Nywele Zilizokuwa Hazikutajwa Katika Sunnah Kama Nywele Za Kifuani
SWALI
ASSALAMU ALAYKUM.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa kaka yetu kuhusu swali hili. Uhakika ni kuwa Uislamu umejengewa katika unadhafa wa kimwili, mavazi, sehemu anayoishi mtu na sehemu nyenginezo. Katika huu unadhafa ni kuchukua udhu, kuoga na kufanya mengineyo kama kukata nywele za kinena, za makapwa, kupunguza masharubu lakini kuacha ndevu. Imechukuliwa kuwa nywele za kifua zitakuwa nyingi na utakuwa huwezi kuweka usafi unaohitajika basi unaweza kunyoa kwani hakuna nasw ya kukataza.
Na Allah Anajua zaidi.