Kujuana Vizuri Kabla Ya Ndoa

SWALI:

 

Asalaam alyekum,

 

Shukran kwa site nzuri sana inatukumbusha mengi waislamu.

Naomba kuuliza mwanamme akikutamkia anataka kukuoa alafu umjibu kwa mfano.. wacha tujuane vizuri kwanza ndio ndoa ifuate ikimaanisha tabia ...

then mwanamme akubali lakini akate mawasiliano mda mchache.... kweli alikuwa na nia ama? Imemtoka rafiki wangu kipenzi naomba msichapishe wa umma.

 

Shukran

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukran kwa swali lako kuhusu mwanamme kumtamkia mwanamke kuwa anataka kumuoa kisha akate mawasiliano.

 

Mwanzo tunatakiwa tufahamu kuwa hakuna katika Uislamu kujuana vizuri baina ya mwanamme na mwanamke kabla ya ndoa.  Linalotakiwa ni kwa mwanamme kuulizia kuhusu anayetaka kumuoa na mwanamke vile vile.  Na zipo njia nyingi za kila mmoja kutumia za kishari’ah kujua kuhusu wapili wake. Baada ya kupata maalumati kuhusiana na hilo basi mwanamme aende akampose mwanamke huyo kishari’ah.

 

Ikiwa mwanamme ametamka kuwa atakuoa kisha akakata mawasiliano ni kuwa mwanamme huyo hakuwa na Niyah ya sawasawa kuhusu suala hilo la ndoa. Kwa hiyo, sasa sahau hilo mpaka atakapokuja kwenu rasmi kutaka kukuposa. 

 

Na akija mwengine ambaye anataka kukuoa kikweli na ana tabia njema basi kubali bila ya tatizo lolote na wala usisite kwa kutaraji yule wa mwanzo labda atarudi au la.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share