Majina Ya Watu Waliojitangazia Unabii Kabla Na Baada Ya Kufariki Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Majina Ya Watu Waliojitangazia Unabii Kabla Na Baada Ya Kufariki

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

 

Swali. Napeda kujua majina ya watu walio Jitangazia Utume Kabla na Baada ya Kifo cha Mtume wetu (Amani ya Allaah iwe juu yake) na nani aliye wauwa au kama walitubia.

 

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Wale waliojidai ni Manabii katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni Musaylamah bin al-Habiyb al-Kadh-dhaab na Twulayhah al-Asadiy.

 

 

Ama wale waliojidai kuwa ni Manabii baada ya kuaga dunia kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), yaani wakati wa Ukhalifah wa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) walikuwa ni al-Aswad al-‘Ansi na Sajaah bint al-Haarith bin Su’ayd.

 

 

Na baada ya hapo wapo waliojidai kuwa wanapata Unabii katika miaka ya baada ya hapo na mpaka wakati wetu huu wako waongo kama hao ambao kudai kwao hivyo ni kutoka nje ya Uislamu kwa sababu dalili tele zimethibiti kuwa hakuna   Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Nabiy wa mwisho katika Ummah huu mpaka Siku ya Qiyaama. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

 

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Ahzaab: 30]

 

Na katika Hadiyth:

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mfano wangu na mfano wa Mananbii wa kabla yangu ni kama mfano wa mtu aliyejenga nyumba akaifanya nzuri na kuipamba isipokuwa sehemu moja ya tofali katika kona. Watu wakawa wanalizunguka na kustaabishwa uzuri wake na husema: “Je, hili tofali litajazwa sehemu yake?” Basi mimi ndio tofali, nami ndiye Nabiy wa mwisho)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share