Amemtamkia Talaka Zaidi Ya Mara Tano Nyakati Mbali Mbali

SWALI:

 

Assalam Aleikum, Sheikh, nina maswali ambayo yamekuwa yakinitatiza kwa mda mrefu sasa, naomba unipe majibu angalau niweze kuridhika, najua kwamba swali langu laweza kuwa limejibiwa hapo mbeleni kwa kuulizwa na mtu mwingine lakini tafadhali naomba nijibiwe one on one at least..Swali lenyewe ni hili. Mume anapomwambia mkewe kwamba "Nimekuacha" au "nimekupa talaka" au sikutaki nenda kwenu kwa zaidi ya mara tano na on different occasions, hukumu ni nini? Talaka huwa imepita au bado? Kila wakati atakaposema hivyo, utaona anajuta na kuniambia kuwa. Amewahi kuniandikia talaka akasema kuwa hakuwa serious ni jokes tu, then mara ya pili, alitype kwa kutumia computer then akanipa, another incident nilikuwa kwenye hedhi then tukatofautiana kiasi, akaniambia kuwa ameniwacha then akasema "Yarrabi, sitaki mke wangu, simtaki kabisa" point yangu is this, amenitajia talaka zaidi ya mara tatu and on different occasions, sasa bado mimi ni mke wake au la?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kupatiwa talaka na mumeo kwa sababu moja au nyengine.

Talaka ni tendo moja ambalo mzaha wake ni ukweli na ukweli wake ni ukweli.

Talaka ni tendo ambalo linasihi ikiwa itakuwa imeandikwa au imesemwa, kukiwa na mashahidi au la.

Talaka ni kitendo ambacho ikiwa kitafanywa wakati mke yuko katika hedhi au tohara basi kitasihi, ingawa yule mume ambaye atampatia mkewe talaka akiwa katika hedhi basi atakuwa amepata dhambi.

 

Idadi ya talaka ni tatu ambayo inatolewa na mume kumpa mkewe. Na hizo talaka tatu hazitolewi kwa mpigo kwa kauli iliyo sahihi zaidi. Mume akitoa talaka ya tatu, huwa wanandoa hao hawawezi tena kuwa ni mume na mke mpaka mke aolewe na mume mwengine kisha aachwe talaka ya kawaida. Allaah Aliyetukuka Anasema:

Talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri… Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Allaah” (al-Baqarah 2: 229 – 230).

 

Kwa kuwa mumeo amekupa talaka zaidi ya tatu hakuna ndoa tena baina yenu hata akijuta namna gani. Linalotakiwa kwa sasa ni wewe kurudi kwenu ungojee neema ya mume mwengine.

 

Ikiwa utabaki kwa aliyekuwa mumeo basi mtakuwa mnazini tu, na zinaa ni dhambi kubwa.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

 

Talaka Ya Mara Tatu

 

Talaka Tatu Pamoja Inakubalika? Mume Hatimizi Zamu Kisha Ametoa Talaka Mara Tatu Kwa Pamoja

 

Mas-ala Ya Talaka Mbali Mbali

 

 

Talaka Tatu Zimepita Lakini Bado Tunatakana

 

Talaka Ziko Aina Ngapi Na Wakati Gani Zinasihi?

 

Kwa Nini Haiwezekani Mke Na Mume Kurudiana Baada Ya Talaka Tatu?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share