Msichana Ameolewa Na Hakukutwa Na Bikra Nini Hukmu Yake?
Msichana Ameolewa Na Hakukutwa Na Bikra Nini Hukmu Yake?
Swali:
Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam
Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa, kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu
Je kuna hukumu yeyote inayohusu kama msichana ameolewa na hakukutwa na bikra.
Natanguliza shukrani zangu kwa Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa na nyinyi pia ndugu zetu wa Alhidaaya. Wabillah Tawfiq
Jibu:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Suala la ubikira ni suala lenye utata mkubwa sana kwenye jamii zetu kwa kiasi ambacho wenye kuoa huwa wakitazama kama wake zao watatoka damu wanapoingiliwa. Na hili si jambo la lazima kwani ni kawaida kwa msichana kutoka damu anapoingiliwa kwa mara ya kwanza lakini wengine wako nje ya ada hii; kwa maana kuwa hawatoki damu wanapoingiliwa kwa mara ya kwanza. Pia wapo wengine wanaopoteza ubikira wao kwa sababu ya kucheza michezo yenye kuwafanya warukeruke au upandaji wa wanyama, na pia uendeshaji baiskeli pia huwezi kumuondoshea msichana ubikira wake kwani ubikira huondoka kwa kukatika kizinda.
‘Alaa kulli haal, yatakiwa ikiwa mume ameoa na akaona kuwa mkewe si bikira na hali aliuliza au alijulishwa kuwa mwanamke anayo bikira, basi anaweza kuzungumza naye kutaka kujua ukweli wa kupoteza kwake ubikira na anapaswa kumwamini analolisema. Vinginevyo anaweza kuamua kukataa kuishi naye kwa sababu anaona atakuwa na wasiwasi kila jjmara kwa kumshuku mkewe. Kwa njia hiyo itabidi mume arudishiwe mahari yake.
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Kumsubiri Bibi Harusi Nje Ya Mlango Kujua Kama Ni Bikra (Kijibu Harusi)
Wanawake Wanaojichua, Bikira Huweza Kuondoka?
Kurudisha Ubikra Haifai Na Ni Udanganyifu
Vipi Atahakikisha Kama Msichana Anayetaka Kufunga Naye Ndoa Ni Bikra; Na Kama Si Bikra Atajua Vipi?
Na Allaah Anajua zaidi