Inafaa Kushirikiana Na Makafiri Kuwachangisha Pesa Waislamu Wenzao Kuzitumia Kwa Siri?
SWALI:
Asalam Aleikum, Natarajia U mzima na Allah s.a.w, Apate kukuhifadhi na kukupa afya. Sheke nilikuwa na swali au ombezi moja na natarajia utanifafanulia au kunijibu hili hoja ambalo linalo ni kera
kuna watu ambao wanaowahubiria wasio kuwa waislamu (wakristo) kupitia kitabu chao, na kupata kuwasilimisha wengi
wasalam aleikum
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kushirikiana kwa Waislamu na Wakristo katika ukusanyaji wa pesa katika mihadhara.
Uislamu umeweka misingi ya ukweli na uaminifu na mlinganiaji Muislamu anatakiwa awe aifanye kazi ya ulinganiaji kwa kufuata maadili bora katika ulinganizi
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitutahadharisha kwa kutuambia: “Mwenye kutudanganya si katika sisi” (Muslim).
Na haifai kwa Muislamu kushirikiana na hata Muislamu mwenziwe licha ya Mkristo katika kuwalaghai na kuwatapeli wanaadamu pesa au kitu chochote kingine. Hivyo, jambo
Na Allaah Anajua zaidi