Mwanamke Kupandikizwa Mimba (IVH) Bila Ya Kujamiiana Na Bila Ya Ndoa Ili Kupata Mtoto
SWALI:
Asalaam alaykum. Mimi nina maswali mawili yahusianayo na watoto;
je ni halali hizi mimba za kupandikizwa kwa mwanamke bila ya tendo la kujamiiana. I mean kuchukua sperm za mwanamme ambaye hamujaoana na kuzipandikiza kwa tumbo la mwanamke (IVF) ili kupata mtoto?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu uhalali wa kupandikiza mimba bila kujamiiana.
Hakika hiyo ni ghushi kubwa
“Mwenye kutudanganya si katika sisi” (Muslim).
Kisha hii ni aina ya ndoa inayofanana na ile ile iliyotajwa na mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kuwa wakati wa ujahiliya mume alikuwa anamwalika mwanamme ambaye ana baadhi ya sifa naye akataka apate mtoto mwenye sifa
Hivyo, kuyatia manii ya mwanamme kwa mwanamke asiye mkewe ni haramu katika shariah ya Kiislamu.
Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo na manufaa zaidi:
Uzazi Wa Kupandikiza Wa Chupa (Test Tube) Unafaa?
Na Allaah Anajua zaidi