Maovu Yanayofanyika Katika Sherehe Za ‘Arusi (Harusi)
Maovu Yanayofanyika Katika Sherehe Za ‘Arusi (Harusi)
Imekusanywa na: Muhammad bin ‘Abdillaah Al-Habdaan
BismiLlaahi Rahmaani Rahiym
Shukrani ni za Allaah na rehma na amani zimfikie Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallaam) na watu wake na Swahaba zake na wanaowafuata hadi Siku ya mwisho.
Amma ba’ad;
Hakika furaha ni utulivu wa mioyo yetu, ni kipumbazo cha macho yetu. Wakati tunaposikia habari ya ‘Arusi (Harusi) kuwa fulani anamuoa fulani, jambo hili ni sababu ya kusimamisha (Sunnah) mwendo Aliouweka Mola na kwa njia hii ndio kuendelea kizazi cha viumbe.
Na kwa njia hio yajulisha uhakika wa umbile lao binaadamu na kawaida yao. Ndani yake yapatikana mema mengi yaliyo matukufu.
Kuna jambo lilolazimisha nafsi, likaumisha moyo na kukata maini. Likaleta fikra nyingi zenye kuleta majuto, nazo ni kuizungusha (kuibadilisha) neema hii ya Nikaah kwa mambo yanayopeleka katika uangamivu. Ikawa ni yenye kuleta ghamu, ikamalizikia hivyo na kutorudi katika hali yake ya asili. Tunawaita kwa kuwaelekeza ndani ya mazungumzo haya huenda tukafaulu na mawaidha yetu yakabadilisha hali zetu katika haya tutakayojulishana.
Kwanza:
Imeenea kwa wanawake wakubwa na wadogo, wawapo katika furaha na mengineyo kwao kuvaa nguo za haraam, zisizo na sifa wala mwenendo unaotakiwa na Shari’ah ya Kiislamu. Ingawa wapo wanaotoa sababu kuwa ‘tupo na wanawake wenzetu peke yetu’.
Katika mavazi yenyewe yasiyofaa ni yale yanayobana mwili na kuufitini, au kuwa wazi juu kifuani ikawa yaonyesha sehemu kubwa ya kifua chake, au mgongo wake, kuna zenye kupasuliwa chini mpaka ikafikia gotini ama karibu ya goti, kuna zilizokuwa nyembamba zinazoonyesha wasifu wa rangi ya mwili wake. Kwa mfano shifoni na suruali ambao ni yenye kuleta matatizo makubwa na machungu mengi.
Imepokewa na Imaam Ahmad katika isnadi yake kutoka kwa Usaamah bin Zayd amesema: “Alinivalisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nguo ya sufi (qubtwiyah) nyepesi yenye kuonyesha, aliyopewa zawadi, nikampa mke wangu aivae. Akaniambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwanini huivai qubtwiyah, nikamwambia ee Rasuli wa Allaah nimempa mke wangu. Akaniambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “muamrishe aiwekee kitu ya kuifunika ndani yake, isije ikaonyesha umbile la mwili wake.”
Nawauliza enyi viongozi, wasimamizi, wachungaji watukufu, kwa nini wasimamizi wanawaruhusu maharimu zao kuvaa nguo za kufedhehesha? Uko wapi uchungaji wakati wa kununua na baada ya kununuliwa?
Ni kwanini hawi na hukumu kiongozi, mchungaji akataka kwa anayemuongoza. Ikiwa ni mkewe amvalie yeye nguo inapokuwa mpya kabla kuvalia watu, ili astarehe kwa kuiona yeye mwanzo. Aionapo ni yenye kukubaliwa na Shari’ah iwe khayr kwake na kumshukuru kwa kufanya jambo zuri na kushonwa inavyotakikana na Shari’ah kwa kuisifu. Aionapo imekhalifu Shari’ah haliridhii Mola Aliyetukuka na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), amsifie kuhusu Dini yake na uzuri anayefuata Shari’ah katika maisha yake kwa kumwambia ‘una nini mwanamke mwema kuvaa nguo nyepesi, nguo ya kupasuliwa, nguo ya kubana, nguo ya wazi hii si katika sifa yako Muuminah...’ Huenda ukitumia njia hizi ukabadilishiwa yaliyo bora.
Njia hizi yaleta mapenzi na kuondosha Munkar akipenda Mola aliyetukuka. Iwapo hutofaulu, waeleze viongozi wa mke (wazazi) japo atalia kwani hiyo ni njia yao inayojulikana kwao. Elewa ewe kiongozi mpendwa, kilio cha kukatazwa shari ni bora kuliko kilio cha kesho chenye kukuingiza katika shari na mwisho usiokuwa na manufaa ila majuto.
Wamelalamika wanawake wema yanayotokea katika ‘Arusi, kutokana na kuvaliwa nguo za wazi, kwa kupatikana wanawake wanaoonekana miili yao na mambo ya aibu ya kufedhehesha yanayotokea.
Ni 'Ulamaa wangapi wanaolitolea fatwa jambo hili kwa uharamu wake, kwa kuweka wazi jambo hilo. Ni jamii ngapi imekuwa wanafanya maasi juu ya maasi, sababu ni kuanza kulihalalisha hili.
Kwa wale wanaoruhusu wanawake na watoto wa kike kuvaa wazi na nguo za kufedhehesha, hawalijui neno la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilolisema kwa maonyo na makemeo kwa kukhofisha hili:
“Sampuli mbili ni watu wa motoni sijawaona: Wanawake wamevaa lakini wako uchi, vimejaa vichwa vyao kama mfano wa nundu ya ngamia kwa kule kufura, hawatoingia peponi wala hawatoisikia harufu yake, inasikika harufu yake mwendo wa masafa kadha wa kadha.” [Imepokewa na Muslim, 1828] Na katika mapokezi ya Imaam Ahmad: “Walaanini, hakika hao wamekwisha laaniwa.”
Wamuogope Allaah(Subhaanahu wa Ta'aalaa) viongozi walioghafilika, na watu wao wauogope ufalme wa Mmoja (Rabb) Aliye na nguvu na adhabu Yake, Siku atakayosimama kila mmoja wetu, Siku ya fazaa (kubabaika) hakutokuwa na mwenye nguvu kumzuia wala mwenye uwezo kutoa nusra, yote hayo uwezo ni Wake. Utapata nani akuokoe Siku hiyo? Tambua ya kuwa tutakapomtii, basi hakuna mfano wake kwa huruma. Usiwe mkaidi ewe mwanaadamu kuipoteza amana uliopewa, ukawa ni mwenye kulichoma ini lako, ukafanya uovu usio mipaka, utarudi wapi?
Pili:
Maovu yanayotokea katika ‘Arusi ni kwa wanawake kutoka nje wakiwa wamejitia manukato (yaani kujifukiza na kutia mafuta mazuri perfume). Huu ni uovu mkubwa wanaoudharau wanawake wengi. Imepatikana makemeo na kuonywa kwa ukali jambo hili lisilotakikana kwa hapa kujadiliana wala kuzozana nalo.
Amesema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Mwanamke yeyote atakaejitia manukato, kisha akatoka akawapitia watu wakaisikia harufu yake huwa amezini.” [Imepokewa na An-Nasaaiy, 1528]
Si mzinifu wa hakika bali wa kufananishwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kule kueneza kwake uovu wake, kutia manukato na kutoka nje ilhali wanaume wakiwa wamependezwa sana na jambo hilo, na kuwafungulia jambo litakalowapeleka katika uzinifu.
Zingatia ewe Muumini haya nitakayoyasema; lau atatoka mwanamke akajitia manukato akikusudia kwenda Msikitini kuswali, je lafaa hilo kwake? Hakika inakutosheleza kukujibia hilo kwa kupitia jibu la ambae haongei kwa mapenzi ya nafsi yake isipokuwa kwa wahyi. Amesema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Mwanamke yeyote atakaetoka kwenda Msikitini, asijitie manukato.” [Imepokewa na An-Nasaaiy, 5131]
Jambo linalostaajabisha ikiwa kwenda nyumba ya Allaah kutekeleza faradhi za Allaah imekatazwa, vipi kwa yule anayejitia manukato akaenda katika sherehe, anawafitini wangapi katika njia yake mpaka afikapo kumbi za starehe?
Tatu:
Ni maovu yanayosikika ndani ya kumbi za starehe (hall) kwa kudumu katika sherehe hizo ngoma na muziki ambao ni upuuzi. Ama kuhudhuria wanamuziki wa kiume na wa kike, ama baadhi ya wanawake makhsusi wanaopiga ngoma na matari wakaimba kwa sauti zikasikiwa na waume, zikawa zimejaa maneno machafu (mabaya), wakaimba waimbaji wabaya na kucheza kwa muziki huo mchezo wa ajabu ama wa kileo (Wakimagharibi ama Mashariki), je waona hii ni sawa ya kuialika Nikaah!?
Utaona yule anayehalalisha mfano wa nyimbo hizi, ni kwa maneno yaliyokuwa na uchache (upungufu) wa hayaa ni uimbaji wenye kelele nyingi.
Rabb Aliyetukuka cheo Chake na yalotakasika majina Yake, ametujuulisha katika Qur-aan uharamu wa nyimbo kwa kukataza uharamu wake, ili kumchunga kila mwenye moyo na masikilizi ya kushuhudia hilo.
Amesema Aliyetukuka:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٦﴾
Na miongoni mwa watu, yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) njia ya Allaah bila elimu, na huichukulia mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha. [Luqmaan: 6]
Hakika aliapa Swahaba mtukufu ‘Abdullaah bin Mas’uud (Radhwiya Allaahu ‘anhu) makusudio ya lahw hapa ni nyimbo.
Imekuja Hadiyth iliyothibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Watapatikana katika Ummah wangu watu watakaohalalisha zinaa na kuvaliwa hariri kwa wanaume, na unywaji wa tembo, ulevi na muziki.” [Imepokewa na Abu Daawuud na Al-Bukhaariy].
Na jengine linalotokea hapo ni uchezaji wa wanawake bila ya mpangilio wa Shari’ah wala uchungaji wa mipaka. Jambo ambalo linaloleta ufisadi, Rabb Anayashuhudia matendo hayo ambayo matokeo yake:
1- Ni wanawake wengi kupata jicho la hasad kwa kuhusudika. Kwani hujitahidi mwanamke kwa bidii zake zote kujionyesha ili watu wamuone (wamtazame yeye) katika mavazi yake na namna alivyojitolea. Imekuja Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) neno lake: “Wengi watakaokufa katika Ummah wangu baada ya maandiko na makadirio ya Allaah ni kwa sababu ya jicho.” Hadiyth hii imo katika Fat-h Al-Baariy ya Ibnu Hajar, 167/1; imo katika Silsilatul-Hadiyth asw-Swahiyhah, 384/2.
2- Ni kupatikana jini kwa kule kucheza ambako kunakojulikana leo na wengi. Hata ikiwa utasalimika na haya nakuuliza: Je tabia hii yatokana na utakaso (twahara) ama hayaa, yamridhisha Rabb wa mbingu na ardhi? Hakika linalohuzunisha sana ni kuwaona wasichana wa Kiislam wako katika tabia (mwendo) huu unaoondosha hayaa na kuondosha utukufu (cheo) cha mtu. Inapokosekana hayaa kwa mwanamke humpeleka yeye katika kila uovu wa maovu na kwenye tabia mbaya za wabaya. Na kinyume chake humuondoshea tabia nzuri na kumpeleka katika mbaya ya wanaosifika vibaya, itaendelea kumuangushia cheo chake na kukifanya cheo chake kuwa ni cha chini cha walio chini.
Amesema kweli ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu):
“Mwenye kuwa na hayaa iliyo kidogo hupungua ucha Mungu wake, na mwenye kupungua ucha Mungu wake hufa moyo wake.”
Kinachomzuia mtu kutenda yaliyoharamishwa ni hayaa, inapozidi hayaa kwake huwa si mwenye kufanya maasi na inapozidi hayaa inaleta taqwa.
Mshairi mmoja amesema:
Huenda uovu ulokuwa nifanyiwe,
Usiwe ni wenye kufanywa ila kwa ajili ya hayaa,
Imekuwa ndio dawa yake kubwa,
Lakini iondokapo hayaa huwa hakupatikani dawa.
Hakika kualikana ‘Arusi Alikokuhalalisha Allaah,
Si huu wanaofanya wengi.
Bali ni yanayopatikana sitara
Na utakaso na kuungana na nyimbo zilotakasika
Na kuwa mbali na maneno mabaya na mambo ya kuangusha cheo.
Ama kupatikana ala za muziki za upuuzi na ubatilifu,
Ni kwa kupiga tari la kishari’ah ambalo liko wazi upande mwengine,
Iwe katika mzunguko wa wanawake pekee, wasisikike na waume.
Ama kulingana na kucheza wanawake mbele ya wanawake, ametoa fatwa Al-‘Allaamah Muhammad bin Swaalih ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: “Kucheza wanawake, hili ni jambo baya hatuwezi kulitolea fatwa ya kulihalalisha kutokana na matokeo yanayotufikia kwa sababu ya kucheza.” [Fataawa Islaamiyah, 187/3].
Hasa katika zama hizi zenye taabu (shida) na kustawi fitna ndani yake.
Nne:
Katika maovu yanayotokea katika sherehe za ‘Arusi ama furaha zetu, ni kuchukuliwa video ama kupigwa picha ndani ya kumbi (hall). Ikiwa ni ‘Arusi ama mengineyo katika mihadhara.
Hili Rabb Analijua zaidi shida na taabu yanayotokea kwa ajili ya hizo! Na matokeo mangapi [mabaya] yaliyotokea? Haya hutokea kwa sababu ya makosa yanayofanywa katika sherehe hizi zao. Ni juu yako uzingatie kwa makini kupitia makosa haya ya kanda za video yanavyoendelea.
Elewa kuwa mwanamke anapokwenda ‘Arusini huwa yupo katika hali gani? Anakwenda ‘Arusini akiwa amejipamba kwa mapambo mazuri, amekuwa anaonekana mzuri. Ni mwanamume gani aliyekuwa na busara atakayetaka Mahaarim zake waonekane na wanaume ajnaby!? Ni wangapi wanaozizungusha hizi kanda? Elewa kuwa ndani kuna sura za wanawake hawajulikani, wanawake wanaojisitiri wasiopenda uovu huu kwa kuwa wao ni wanawake wema.
Huonekana wanawake hawa kila pande kwa kusahilisha na kudharau katika akili zao. Jambo la kupiga picha na kuchukuliwa kwa video, likaleta khasara na majuto mengi ndani yake.
Tano:
Katika maovu ya sherehe za ‘Arusi ni kuchelewa kukaa sana usiku, jambo linalofanya kuikosa Swalaah ya Alfajiri - ama kuichelewesha kwa wakati wake uliopangwa na Shari’ah, katazo lililoteremshiwa Aayah katika Qur-aan kuwaonya na kuwakemea kwa kutamka maneno makali na lugha nzito isiyofahamika ila kwa wale wenye akili pekee:
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾
Basi Ole kwa wanaoswali ... Ambao wanapuuza Swalaah zao. [Al-Maa’uwn: 4-5]
Yaani wanaswali baadhi ya Swalaah na kuacha nyingine.
Amesema Masruuq (Rahimahu Allaah), maana ya hii Aayah - yaani hawaziswali Swalaah kwa wakati wake ulioamrishwa na kuwekwa na Shar’iah.
“Hakika kuchelewesha Swalaah ni kosa kubwa lenye uzito kwa kila aliye na hisia kulikisia hilo, na ni kosa lenye kufedhehesha (kumtia aibu) kila mtendaji kitendo hicho kibaya. Wala hayatomfalia majuto yake wala kutoa sababu zake (nyudhuru) atakaposimama mbele ya Rabb Mmoja Mwenye nguvu (siku ya Qiyaamah).”
Waonaje... Waonaje... Wewe unayelala bila kuiswali Swalaah ya Alfajiri!? Waona vipi adhabu inayokungojea, nawe umeghafilika nayo? Hujui utaipata vipi adhabu hii, na imetayarishwa vipi kwako wewe? Muogope Rabb wako, uziepuke sababu zitakazokufanya uache Swalaah ama kuichelewesha. Adhabu hii ni jambo linalopatikana lakini lenye khatari, na ni haki inayopatikana kwa waume na wake.
Sita:
Katika yanayopatikana kwenye sherehe za ‘Arusi ni pale matokeo yatokeapo wakati wa wanawake kwenda zao. Utaona mambo ya kukata maini kwa fursa na nafasi zenye khofu zenye uzito wa jambo linaloonekana. Utaona mwanamke anatoka mikono yake ipo wazi inaonekana, ameyadhihirisha macho yake. Amevaa buibui jepesi lilojaa manukato na mapambo (lililo rembeshwa), bali hilo buibui lipo mabegani apitiapo mtu ana kuachia harufu manukato kila mwanamume aliyekuja kuchukua jamii yake, anayesubiri mlangoni katika ukumbi (hall) aipata harufu hiyo.
Bila ya shaka yoyote haya ni maradhi yanayotaka dawa. Hivyo, ninatoa nasaha kwa yafuatao huenda ikawa dawa.
1) Ajue kiongozi kila anaemuongoza atokapo (mkewe, bintiye n.k.) nyumbani, awe amejisitiri vizuri inavyohitajika katika hijaab yake.
2) Wanaume wainamishe macho mbele ya wanawake wanaotoka wazi kwa kuzidhihirisha tupu zao. Tambua kuwa utakapofedhehesha kuangalia tupu ya mwenzako basi umehalalisha kuangaliwa ya kwako pia.
Elewa kuwa unapokiangusha cheo cha mtu, ndivyo kinavyoanguka chako – ‘Kama utavyokopesha ndivyo utakavyolipwa.’
Kuna mtu alimuuliza Junayd utanisaidia vipi katika kuinamisha macho? Akamjbu kwa kumuambia “kuwa na ujuzi (kuwa na elimu)”. Yule anayeangalia kukuangalia wewe, elewa kuwa umetangulia wewe kuangalia yale anayoangalia yeye (yaani hupata malipo) huwa ni malipo.
Akasema mwenye kumsifu kwa urefu Sulaymaan bin ‘Aliy: “Ameniwaidhi mimi, akasema: Unapofanya maasi kwa siri ukajua kuwa Mola akuona, umefanya makosa makubwa kwa jambo hilo (kwa dhana hiyo). Na iwapo utadhania kuwa Mola hakuoni basi elewa kuwa umekufuru.
3) Utapatikana uwanja mkunjufu wa kuingia ukumbini (hall). Kuwe na ukuta (fence) utakaozunguka kwenye mlango lizuie kukaribia kufikia mlangoni. Ipatikane mwanamke kutoka kwa utulivu, ili kiongozi wake ampate kwa wepesi anapofika kumchukua.
4) Wanaume wawepo upande mmoja. Apatikane mtayarishi wa kuita, awe karibu nao wanaume, mbali na mlango wa ukumbi (hall), kila anapotoka mwanamke amfuate kiongozi wake ili kusipatikane msongamano, kwani kuuzunguka ukumbi wanaume katika mlango kunamzuia na kumpa dhiki mwanamke wakati wa kutoka, kwa kuwa ni lazima awapitie wanaume, jambo ambalo halipendezi katika Shari’ah bali ni makosa.
Fatwa:
Aliulizwa Shaykh ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah),
“Je inafaa mwanamke kwenda katika sherehe za ‘Arusi iwapo kutakuwa kunapatikana humo baadhi ya maovu, kama vile ngoma, kucheza, kuvaa wazi. Je kiongozi ana chumo katika dhambi hizi mfano wa mzazi, ama mume anapotoa ruhusa kwenda katika sherehe hiyo? Na inakuaje hukmu yake ikiwa mualiko ni wa jamaa, akaogopea asipohudhuria italeta vita na kukata kizazi? Nipe fatwa, nakutakia malipo, Mola Aakujazi khayr.
Jawabu:
“Ikiwa ‘Arusi ni ukumbi kama hivyo ulivyoutaja katika swali, hakika haifai mtu kuitika mwito huo, isipokuwa ikiwa kuitikia kwake ataweza kuondosha Munkar huo ama maovu hayo.
Iwapo atakwenda kwa kuitikia mwaliko wala hatokua na uwezo wa kuondoa maovu hayo, haifai kwake kuhudhuria mwaliko kama huo ulojaa maovu, wala si halali kwa yeyote kumruhusu mkewe ama mtoto wake ama yeyote anayemuongoza kuitikia mwaliko kama huu, na asemapo kuwa anaitikia kwa kuwa lisitokee la kukosana ama kuteta, twasema: hata anapoitikia mwito kama huo, hilo analolikhofia litatokea kwa kule kumuasi Rabb katika sherehe hiyo ulioisifia, haina usawa wala umuhimu wa kuitikia mwito huo, na watakapoteta na asiyehudhuria mwito huo, elewa kwamba madhambi ni yao wenye sherehe hiyo.
Si kwa yule anayezikataa na kuziepuka sherehe hizo, yeye huwa hana dhambi ya aina yoyote.”
Ndugu Muislamu, hili ndilo ninalolitaka ulipelekee maangalizi yako kwenye jambo hili, pamoja na kuwaidhika na iwe manufaa kwa Waumini. Kwani Muumini ni kioo cha Muumini mwenzake, Waumini huwa wananasihiana.
Mwisho nawaachia kwa Allaah, kwani hapotei mwenye kuachiwa Kwake Yeye. Namuomba Rabb Awasaidie kutekeleza amana zenu, Rabb Awe Hifadhi, Awachunge na Aziweke khatua zenu katika mambo ya khayr.