Kumlaani Shaytaan Katika Swalaah

 

 

Kujikinga Na Shaytaan Katika Swalaah Anapochochea

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, kusema A'udhu Billahi Mina-Shaytwaanir-Rajiym katika Swalah inafaa?  

 

 

 

JIBU

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Anza kwanza kabla ya Swalaah kuomba kinga dhidi ya shaytwaan kwa kusema kama ilivyothibiti katika Sunnah:

 

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّـيْطانِ مِنْ نَفْخِـهِ وَنَفْـثِهِ وَهَمْـزِه

Najikinga na Allaah kutokana na shaytwaan, na kibri yake, na kupulizia kwake na kutia kwake wasiwasi (katika nyoyo za binaadamu)

 

Ikiwa katikati ya Swalaah shaytwaan anakupoteza basi tema mate kidogo tu ya kupulizia  upande wa kushoto wa bega lako na sema mara tatu:

 

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّـيْطانِ الرَّجِيم

Najikinga na Allaah kutokana na shaytwaan, aliyefukuziliwa mbali na kulaaniwa.

 

Kisha endelea na Swalaah yako bila ya kuanza upya, kwani huyo ni shaytwaan anayeitwa Khinzab ambaye anamtia mtu wasiwasi katika Swalaah na wakati wa kusoma Qur-aan kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

عن عُثْمَانَ بْن أَبِي الْعَاصِ رضي الله عنه أنه أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ حَالَ بَيْنِي وَبَيْنَ صَلَاتِي وَقِرَاءَتِي يَلْبِسُهَا عَلَيَّ: فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((ذَاكَ شَيْطَانٌ يُقَالُ لَهُ خَنْزَبٌ، فَإِذَا أَحْسَسْتَهُ فَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْهُ وَاتْفِلْ عَلَى يَسَارِكَ ثَلَاثًا)) قَالَ: فَفَعَلْتُ ذَلِكَ فَأَذْهَبَهُ اللَّهُ عَنِّي .

‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika shaytwaan kanijia baina yangu na Swalaah yangu na kisomo changu akinivaa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema ((Huyo ni shaytwaan anayeitwa Khanzab, basi ukimhisi jikinge naye kwa Allaah, na tema mate upande wa kushoto kwako  mara tatu)). Akasema: Nikafanya hivyo basi akaniondoka shaytwaan. [Muslim]

 

   

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share