Keki Ya Tende Bila Siagi, Mayai Wala Maziwa (Vegan)
Keki Ya Tende Bila Siagi, Mayai Wala Maziwa (Vegan)
Vipimo
Unga - 1 ½ kikombe
Sukari - 1 kikombe
Tende - ½ kikombe
Maji au juisi ya orengi - 1 kikombe
Mafuta ya mboga (vegetable oil) - ¼ kikombe
Baking Soda - 1 kijiko cha chai
Baking Powder - 1 kijiko cha chai
Chumvi - ½ kijiko cha chai
Vanilla - ½ kijiko cha chai
Mdalasini unga - ½ kijiko cha chai
Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai
Siki - 1 kijiko cha chai
Sukari laini (icing sugar) - 1 kikombe
Maji - 2 vijiko vya kulia
Namna Ya Kutuayarisha Na Kupika:
- Washa jiko la tanuri (oven) moto wa 350°F
- Paka mafuta au siagi chombo cha kupikia keki
- Chambua tende kisha isage kwa maji au juisi ya orengi iwe rojo (puree)
- Katika bakuli kubwa, changanya vitu vikavu vyote.
- Katika bakuli dogo, changanya vitu vya maji vyote.
- Changanya vyote pamoja kwa mwiko wa moto (electrical mixer) au mchapo wa mayai.
- Mimina katika treya ya keki uliyoitayarisha kisha ipike ndani ya oveni kwa muda wa dakika 30-35.
- Ikiiva, itoe kisha iache ipoe kisha mwagia icingi sugar uliyoitayarisha.
Namna ya kutayarisha frosti ya icing sugar (icing sugar frost)
- Changanya icing sugar na maji kidogo kidogo kiasi cha kuchanganya vizuri kisha mwagia juu ya keki.
Kidokezo:
Keki inawafaa wenye matatizo ya mzio (allergy) ya vitu vinavyotokana na maziwa (dairy), mayai n.k. Inawafaa khasa watoto wasioweza kula keki za kawaida.