Al-Uswuwl Ath-Thalaathah (Misingi Mitatu) - الأُصًولُ الثَّلاثة (Word Doc) Chapisho La 4 Kimehaririwa 1438H (2017M)
Sikiliza Matn Ya Al-Uswuwl Ath-Thalaathah
الأُصُولُ ألثَّلاَثَة
للإمامِ مُحَمَّد بِن عَبْدِالوَهَّابِ
AL-USWUWL ATH-THALAATHAH
(MISINGI MITATU)
Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab
Mfasiri: Ummu Iyyaad
الأُصُولُ ألثَّلاَثَةُ
Al-Uswuwl Ath-Thalaathah
(Misingi Mitatu)
Mwandishi:
Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab
Mfasiri:
Ummu Iyyaad
Chapisho la 4 Kimehaririwa: 1438H (2017M)
YALIYOMO:
Historia Fupi Ya Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab ……. 5
Mas-ala Manne ……………………………………………………… 11
Msingi Wa Kwanza: Kumjua Rabb ………………………………… 16
Msingi Wa Pili: Kujua Dini Ya Kiislamu Kwa Dalili ………………. 24
Msingi Wa Tatu: Kumjua Nabiy Wenu Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)
……………………………………………………………… 32
Historia Fupi Ya Imaam Muhammad Bin Abdil-Wahhaab[1]
Asili yake
Jina lake ni Abul-Husayn Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab bin Sulaymaan bin ‘Aliy Musharrif Al-Wuhaybiy. Kabila lake ni Bani Tamiym. Amezaliwa mwaka 1115 H (1704 M) katika mji ya ‘Uyaynah kijiji cha Yamaamah ndani ya Najd, kaskazini Magharibi ya mji wa Riyadhw, Saudi Arabia. Ametoka katika familia ya Wanavyuoni kwani baba yake ‘Abdul-Wahhaab alikuwa ni Mwanachuoni maarufu wa Najd na Qaadhwi wa mji huo.
Elimu Yake
Alijifunza kusoma Qur-aan alipokuwa na umri mdogo na akaihifadhi akiwa chini ya umri wa miaka kumi. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Alimjaalia kuwa na uhodari na akili nzuri, wepesi wa kufahamu na kumaizi jambo au somo. Alipendezewa mno kusoma kazi za Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibnul-Qayyim (رحمهما الله).
Alifanya bidii kwenye masomo yake na kuendelea kujifunza chini ya usimamizi wa baba yake. Akajifunza elimu ya Dini chini ya Wanavyuoni walioko mjini mwake wakiwemo baba yake na ‘ammiy yake. Alisafiri kutoka kwenda Madiynah kusoma chini ya Wanavyuoni wakubwa wa huko wakiwemo; Shaykh ‘Abdullaah bin Ibraahiym bin Ash-Shamariyyi, na Mwanachuoni maarufu wa India Shaykh Muhammad Hayaat Al-Sindi. Alikwenda Makkah pia na alitekeleza Hajj. Hatimaye akaelekea Baswrah (Kaskazini Iraq) kutafuta elimu zaidi akasoma chini ya Wanavyuoni wa huko akawa maarufu kwa mijadala baina yake na Wanavyuoni.
Harakaat Na Mitihani
Watu wa Najd walikuwa katika shirki na bid’ah (uzushi). Walikuwa wakiabudu miungu mingi na kuabudu makaburi, miti, mawe, mapango, majini na mashaytwaan, waja wema waliojulikana kama ni mawalii. Uchawi na unajimu (utabiri wa nyota) ulisambaa pia. Hakuna aliyekataza ‘iIbaadah potofu hizo kwani watu walikuwa katika kuchuma manufaa na starehe za dunia zaidi na wakakhofia kuyapoteza hayo. Hivyo Shaykh akaona umuhimu mkubwa uliohitajika kuwarudisha watu katika manhaj ya Qur-aan na Sunnah. Akaanza kuwalingania watu katika Tawhiyd - kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) bila ya kumshirikisha na lolote katika ‘ibaadah. Akaazimia kujitumikisha peke yake kwa uvumilivu katika konde. Akajua hakuna lolote kitachofaulu kufanyika ila jihaad katika njia ya Allaah.
Shaykh alikumbana na mitihani, misukosuko, na vitisho, lakini alikuwa ameshategemea hali hiyo kumfikia na alikuwa tayari kukabaliana nayo kwani alitambua kuwa hilo ni jambo lisiloepukika kwa kila mlinganiaji kwani ndio hali waliyokutana nayo Manabii wote, na Salafus-Swaalih (waja wema waliotangulia).
Miongoni mwa mitihani aliyokumbana nayo ni kutokana na Wanavyuoni wadhaifu wasiokuwa na hoja ambao walimpinga na kumfanya akabiliane na misukosuko, vitisho na kukasirikiwa. Pia alikabiliana na misukosuko na mateso chini ya mikono ya madhalimu wa Huraymilaa. Na alipowashawishi watawala wahukumu madhalimu kwa Shariy’ah ya Kiislamu, ilisababisha baadhi ya watu kuyaweka maisha yake hatiani lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Alimnusuru.
Aliamua kurudi kwao ‘Uyaynah, ambako kipindi hicho kulikuwa chini ya utawala wa mtoto wa Mfalme ‘Uthmaan bin Muhammad bin Mu’ammar, ambaye alimpokea Shaykh kwa ukarimu na kumuahidi kumuunga mkono na kumsaidia kuwaita watu katika Uislam. Akaendelea kufundisha na kutoa da’wah hatimaye akashawishika kidhati na kwa vitendo kuondoa dini ya miungu mingi pale alipoona baadhi ya watu ni wagumu kurudi katika Uislamu. Aliweza kumshawishi gavana wa mji huo kulivunja zege lililojengewa juu ya kaburi la Zayd bin Al-Khattwaab ambaye alikuwa ni kaka wa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنهما). Akavunjavunja mangome mengineyo, mapango, miti n.k. Akaamrisha Shariy’ah ya Kiislamu itekelezwe kama kumpiga mawe hadi afe mwanamke aliyekiri uzinifu.
Shaykh aliendelea na harakati zake za kauli na ‘amali ambazo zilimfanya azidi kuwa maarufu. Hatimaye akawa Jaji (Qaadhwiy) wa mji wa ‘Uyaynah. Lakini hakuweza kuendelea hapo kwani Mfalme alishawishiwa na viongozi wa miji ya jirani amuue Shaykh kwa vile hawakupendezewa na da’wah yake. Ikabidi afukuzwe katika mji huo.
Akakaribishwa mji wa Ad-Dir’iyyah ambao ulikuwa ni jirani yake. Huko akakaribishwa ingawa kwanza alitiliwa shaka. Alifikia kwa mja mwema aliyempokea ila alimkhofia kutokukubaliwa na mtoto wa Mfalme Muhammad bin Sa’uwd. Habari zikamfikia kwanza mke wa Ibn Sa’uwd ambaye alikuwa mkarimu na mwenye taqwa. Akamfahamisha mumewe kwa kumwambia, “Hii tawfiyq kubwa umeletewa kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) mtu ambaye anawaita watu katika Uislamu, anawaita katika Qur-aan na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Tawfiyq iliyoje? Mkimbilie haraka na umuunge mkono wala usimpinge au kumkataza kwa hayo”. Muhammad Ibn Sa’uwd akakubali ushauri wa mkewe na akaenda kwa Shaykh na akafanya mkataba naye kwamba asiondoke nchini hapo. Ndipo Shaykh akaweka makazi yake hapo na kuendelea na da’wah. Akaendelea na harakati za da’awah hapo Dar’iyyah. Akaheshimika na kupendwa mno na akaungwa mkono na watu. Da’wah yake iliwaathiri na kuwapendezea mno watu. Ikaenea katika nchi za Kiislamu na nyinginezo. Wakimiminika watu kufika hapo Dar’iyyah kujifunza kwake.
Kama ijulikanavyo kila jema halikosi mitihani. Wakatokeza wapinzani na waliokuwa na chuki naye. Kulikuweko waliompinga da’wah yake ya kuondosha shirki na bid’ah na kuwaita watu katika Tawhiyd. Na wengineo waliompinga kabisa ni kwa sababu ya kuhofu kufukuzwa katika nafasi au vyeo vyao vya kazi. Kwa hiyo wengine walimpinga kwa ajili ya Dini, na wengine walimpinga kisiasa. Wapinzani wake walimzushia ya kumzushia walifika hadi kudai kwamba Shaykh alikuwa ni mfuasi wa Khawaarij. Na mara nyingine wakimlaumu bure bila ya dalili na nje ya upeo wa elimu zao. Hivyo yakaweko malumbano na majibishano yaliyoendelea katika mijadala kadhaa. Shaykh aliwaandikia kuwajibu madai yao, na wao walimrudishia majibu na yeye akawa akiwathibitishia ufahamu wao mbaya wa shariy’ah na Dini kwa ujumla kwa dalili. Ndipo wingi wa maswali na majibu yakawajumuisha watu na wakazidi kuongezeka. Baadhi ya mijadala hiyo iliandikwa na kuchapishwa katika vitabu.
Athari Ya D’awah Yake
Da’wah yake ya takriban miaka 50 imedhihirika na kuleta athari kubwa kwanza kwa Waislamu wa zama hizo. Watu waliacha kuabudu makaburi, miti, mawe, majini, waliacha utabiri wa nyota na kila aina ya shirki. Imewatoa pia watu katika ujinga wa kufuata mila za mababu bila ya dalili. Maamrisho ya mema na makatazo ya maovu yakalinganiwa katika Misikiti. Na hapo msimamo wa Qur-aan na Sunnah ukahuishwa na shirki na bid’ah zikatoweka. Amani na utulivu ukawafunika watu kila mahali. Na mpaka sasa da’wah yake imekuwa na umuhimu mkubwa katika jamii ya Kiislamu. Vijana khasa kutoka nchi za Magharibi na zaidi wale wanaosilimu wamekuwa na hamasa na shauku kubwa ya kujifunza Dini iliyo sahihi na si ile iliyochanganywa na shirki na bid’ah. Kwa hiyo, mafundisho ya msimamo wake wa Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah yamekuwa kipaumbele katika lengo la kutafuta elimu kwa Waislamu watakao na wapendao haki.
Kazi Zake
Ameandika vitabu vingi vya mafunzo mbali mbali lakini alitilia mkazo zaidi katika somo la Tawhiyd na ‘Aqiydah. Na alitumia hikmah ya kuandika vitabu vidogo vidogo lakini vilivyokusanya nukta muhimu kabisa. Vilikuwa ni mukhtasari wa maudhui aliyotaka kuidhihirisha. Na vitabu hivyo vimekuja kufafanuliwa kwa kushereheshwa na ‘Ulamaa kadhaa na vimekuwa vina umuhimu mno katika vyuo vya Kiislamu vinavyofuata mwendo wa Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah.
Vifuatavyo ni baadhi ya vitabu vyake maarufu. Vinne vya mwanzo ni ambavyo mashuhuri zaidi. Na vinginevyo vimekusanywa na kujumuishwa katika ‘Maj’muw’at Mu-allafaatil-Imaam Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab’.
1. Kitaabut-Tawhiyd - kitabu hiki kimekuwa mashuhuri mno na kimeenea sana na somo lake limekuwa ni lenye kutoa mafunzo muhimu kuhusu kumpwekesha Allaah na kuepukana na shirki.
2. Al-Uswuul Ath-Thalaathah – kitabu kitoacho mafunzo kuhusu asili au misingi ya Uislamu.
3. Al-Qawaaid Al-Arba’ - kinatoa mafunzo ya kanuni za ufahamu wa shirki kwa ujumla.
4. Kashf Ash-Shubuhaat - kinakanusha hoja zinazojulikana na watetezi wa shirki na bid’ah.
5. Mukhtaswar Al-Inswaaf was-Sharh Al-Kabiyr
6. Mukhtaswar Zaad Al-Ma’aad
7. Mukhtaswar As-Siyrah
8. Mukhtaswar al-Fat-h
9. Masaail Al-Jaahiliyyah
10. Adaab Al-Mashiy ilaa as-Swalaah
11. Nawaaqidhw Al-Islaam
Wanafunzi Wake
Alikuwa na wanafunzi wengi mno. Miongoni mwao ni watoto na wajukuu wake ambao waliendeleza kazi yake ya da’wah na Jihaad katika njia ya Allaah, walifungua vyuo karibu na kwao wakifunza watu masomo ya Dini. Kati ya watoto wake ni Husayn, ‘Aliy, ‘Abdullaah na Ibraahiym. Na kati ya wajukuu wake ni ‘Aliy bin Husayn, na pia ‘Abdur-Rahmaan bin Hasan aliyeandika kitabu cha ‘Fat-h Al-Majiyd Sharh Kitaab At-Tawhiyd’. Wanafunzi wake wengineo ni ‘Abdul-‘Aziyz bin Muhammad bin Sa’uwd, Hamad bin Naaswir bin Mu’ammar na ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah bin Husayn.
Familia Yake
Alikuwa na watoto sita; Husayn, ‘Abdullaah, Hasan, ‘Aliy, Ibraahiym, ‘Abdul-‘Aziyz. Shaykh anatokana na kizazi kinachojulikana kwa ‘Aal-Shaykh’ ambacho kimetoa Wanavyuoni kadhaa akiwemo Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aal-Shaykh aliyekuwa Mufti mkuu wa awali Saudi Arabia na Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Aal-Shaykh ambaye ni Mufti mkuu wa sasa.
Kifo Chake
Alifariki mwaka 1206 H (1792 M) akiwa na umri wa miaka 91. Rahmah za Allaah ziwe juu yake na Allaah Amruzuku Jannah ya Firdaws. Aamiyn.
الأُصُولُ ألثَّلاَثَة
للإمامِ مُحَمَّد بِن عَبْدِالوَهَّابِ
AL-USWUWL ATH-THALAATHAH
(MISINGI MITATU)
Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمًنِ الرَّحيم
اعْلمْ رَحِمَكَ اللهُ أَنَّهُ يَجِبُ عَلَيْنَا تَعَلُّمُ أَرْبَع مَسَائِلَ:
Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.
Fahamu, Allaah Akurehemu, kwamba ni wajibu wetu kujua mas-alah manne:
المسألة الأُولَى: الْعِلْمُ:
Suala la kwanza: Elimu:
وَهُوَ مَعْرِفَةُ اللهِ، وَمَعْرِفَةُ نَبِيِّهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) وَمَعْرِفَةُ دِينِ الإِسْلامِ بالأَدِلَّةِ.
Nayo ni elimu ya kumjua Allaah, na elimu ya kumjua Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na elimu ya kuijua Dini ya Kiislamu kwa dalili.
المسألة الثَّانِيَة :الْعَمَلُ بِهِ.
Suala la pili: Kuifanyia kazi.
المسألة الثَّالِثَةُ :الدَّعْوَةُ إِلَيْهِ.
Suala la tatu: Kuilingania.
المسألة الرَّابِعَةُ :الصَّبْرُ عَلَى الأَذَى فِيهِ.
Suala la nne: Kuwa na subira katika maudhi yatakayopatikana ndani yake.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْعَصْرِ ﴿١﴾ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾
Kwa Jina la Allaah, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.
((Naapa kwa Al-‘Aswr (zama). Hakika mwana wa Aadam bila shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana haki na wakausiana subira)) [2]
قَالَ الشَّافِعيُّ (رَحِمَهُ اللهُ): لَوْ مَا أَنْزَلَ اللهُ حُجَّةً عَلَى خَلْقِهِ إِلا هَذِهِ السُّورَةَ لَكَفَتْهُمْ.
Imaam Ash-Shaafi'iyy(رحمه الله) amesema: “Lau kama Allaah Asingeliteremsha hoja kwa viumbe Vyake isipokuwa Suwrah hii, basi ingeliwatosheleza.”
وَقَالَ البُخَارِيُّ رَحِمَهُ اللهُ: بَابُ: العِلْمُ قَبْلَ القَوْلِ وَالْعَمَلِ.
Na Al-Bukhaariy(رحمه الله) amesema katika Baabul-’Ilm qablal-qawli wal-‘amal “Mlango wa elimu kabla ya kauli na ‘amali”.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ
((Basi jua kwamba laa ilaaha illa-Allaah, hapana muabudiwa wa haki ila Allaah na omba maghfirah kwa dhambi zako.))[3]
فَبَدَأَ بِالْعِلْمِ قَبْلَ القَوْلِ وَالعَمَلِ.
Akaanza kwa elimu kwanza kabla ya kauli na ‘amali.
اعْلَمْ رَحِمَكَ اللهُ أَنَّه يَجِبُ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ وَمُسْلِمَةٍ، تَعَلُّمُ هَذِهِ الثَّلاثِ مَسَائِل، والْعَمَلُ بِهِنّ:
Fahamu Allaah Akurehemu, kwamba ni wajibu kwa kila Muislamu mwanamme na Muislamu mwanamke, kujifunza mas-alah haya matatu na kuyafanyia kazi:
الأُولَى: أَنَّ اللهَ خَلَقَنَا، وَرَزَقَنَا، وَلَمْ يَتْرُكْنَا هَمَلا، بَلْ أَرْسَلَ إِلَيْنَا رَسُولاً، فَمَنْ أَطَاعَهُ دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَاهُ دَخَلَ النَّارَ.
La kwanza: Kwamba Allaah Ametuumba, na Anaturuzuku, na Hakutuacha bure bali Ametutumia Rasuli. Basi atakayemtii ataingia Jannah, na atakayemuasi ataingia motoni.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا ﴿١٥﴾ فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا ﴿١٦﴾
((Hakika Sisi Tumekutumieni Rasuli awe shahidi juu yenu, kama Tulivyotuma Rasuli kwa Fir’awn. Lakini Fir’awn alimuasi huyo Rasuli, Tukamshika kwa maangamizi makali mno))[4]
الثَّانِيَةُ: أَنَّ الله لا يَرْضَى أَنْ يُشْرَكَ مَعَهُ أَحَدُ فِي عِبَادَتِهِ، لا مَلَكٌ مُقَرَّبٌ، وَلا نَبِيٌّ مُرْسَلٌ.
La pili: Kwamba Allaah Haridhii kushirikishwa pamoja Naye yeyote yule katika ‘ibaadah Yake, ikiwa ni Malaika aliyekurubishwa, wala Nabiy aliyetumwa kuwa Rasuli.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا ﴿١٨﴾
((Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah))[5]
الثَّالِثَةُ ُ: أَنَّ مَنْ أَطَاعَ الرَّسُولَ، وَوَحَّدَ اللهَ لا يَجُوزُ لَهُ مُوَالاةُ مَنْ حَادَّ اللهَ وَرَسُولَهُ، وَلَوْ كَانَ أَقْرَبَ قَرِيبٍ.
La Tatu: Kwamba Atakayemtii Rasuli, na Akampwekesha Allaah, haijuzu kwake kufanya urafiki na ushirikiano na yule anayempinga Allaah na Rasuli Wake hata akiwa ni jamaa wa karibu.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٢٢﴾
((Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda ambaye anapinzana na Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao iymaan, na Akawatia nguvu kwa Ruwh (Wahyi) kutoka Kwake, na Atawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu))[6]
اعْلَمْ أَرْشَدَكَ اللهُ لِطَاعَتِهِ، أَنَّ الْحَنِيفِيَّةَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ: أَنْ تَعْبُدَ اللهَ وَحْدَهُ، مُخْلِصًا لَهُ الدِّينَ. وَبِذَلِكَ أَمَرَ اللهُ جَمِيعَ النَّاسِ، وَخَلَقَهُمْ لَهَا.
Fahamu, Allaah Akuongoze katika utiifu Wake, kwamba al-Hanifiyyah (kuelemea Dini ya haki na kujiepusha na dini potofu) ni Dini ya Ibraahiym. Umwabudu Allaah Pekee ukimtakasia Dini Yake, na kwa hilo Allaah Amewaamrisha watu wote, na Amewaumba kwa sababu hiyo.
كَمَا قَالَ تَعَالَى:
Kama Anavyosema Ta’aalaa:
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
((Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu))[7]
وَمَعْنَى ((يَعْبُدُونِ)) :يُوَحِّدُونِ، وَأَعْظَمُ مَا أَمَرَ اللهُ بِهِ التَّوْحيِدُ، وَهُوَ :إِفْرَادُ اللهِ بِالْعِبَادَةِ. وَأَعْظَمُ مَا نَهَى عَنْه الشِّركُ، وَهُوَ: دَعْوَةُ غَيْرِهِ مَعَهُ.
Na maana ya ((waniabudu)) ni: Wanipwekeshe. Na jambo kuu kabisa Aloamrisha Allaah ni At-Tawhiyd ambayo ni: Kumpwekesha Allaah katika ‘ibaadah. Na jambo kuu kabisa Alokataza ni shirki, ambayo ni: kumuomba mwengine pamoja Naye.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ
((Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote))[8]
فَإِذَا قِيلَ لَكَ: مَا الأُصُولُ الثَّلاثَةُ التِي يَجِبُ عَلَى الإِنْسَانِ مَعْرِفَتُهَا؟
Basi utakapoulizwa: “Nini Al-Uswuwul ath-Thalaathah (misingi mitatu) ambayo mwana wa Aadam anawajibika kuifahamu?”
فَقُلْ :مَعْرِفَةُ الْعَبْدِ رَبَّهُ، وَدِينَهُ، وَنَبِيَّهُ مُحَمَّدًا صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ.
Sema: “Mja kumjua Rabb wake, na Dini yake, na Nabiy wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
الأصْلُ الأوَّلُ: مَعْرِفَةُ الرَّب
Msingi Wa Kwanza: Kumjua Rabb:
فَإِذَا قِيلَ لَكَ :مَنْ رَبُّكَ؟
Basi utakapoulizwa: “Nani Rabb wako?”
فَقُلْ: رَبِّيَ اللهُ الَّذِي رَبَّانِي، وَرَبَّى جَمِيعَ الْعَالَمِينَ بِنِعَمِهِ، وَهُوَ مَعْبُودِي لَيْسَ لِي مَعْبُودٌ سِوَاهُ.
Sema: “Rabb wangu ni Allaah Aliyenilea na Aliyewalea walimwengu wote kwa neema Zake. Naye Ndiye Ninayemwabudu, na sina mwengine ninayemwabudu.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
((AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu))[9]
وَكُلُّ مَنْ سِوَى اللهِ عَالَمٌ، وَأَنَا وَاحِدٌ مِنْ ذَلِكَ الْعَالَمِ.
Na kila kitu kisichokuwa Allaah, ni kilichoumbwa nami ni mmojawapo katika kilichoumbwa.
فَإِذَا قِيلَ لَكَ: بِمَ عَرَفْتَ رَبَّكَ؟
Basi utakapoulizwa: “Umemjuaje Rabb wako?”
فَقُلْ: آيَاتِهِ وَمَخْلُوقَاتِهِ، وَمِنْ آيَاتِهِ: اللَّيْلُ، وَالنَّهَارُ، وَالشَّمْسُ، وَالْقَمَرُ، وَمِنْ مَخْلُوقَاتِهِ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرَضُونَ السَّبْعُ وَمَنْ فِيهِنَّ، وَمَا بَيْنَهُمَا.
Sema: “Kutokana na Aayaat (ishara) Zake na Alivyoviumba. Na miongoni mwa Aayaat Zake ni: Usiku, mchana, jua, mwezi. Na miongoni mwa Alivyoviumba ni mbingu saba na ardhi saba, na kila kilichokuwemo ndani yake na baina yake”
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿٣٧﴾
((Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake, ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Msisujudie jua wala mwezi; bali msujudieni Allaah Ambaye Aliyeviumba ikiwa Yeye Pekee mnawambudu))[10]
وَقَوْلُهُ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾
((Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arshi;[11] Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na (Ameumba) jua na mwezi na nyota (vyote) vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake Pekee uumbaji na amri. Tabaaraka Allaah, Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu))[12]
وَالرَّبُ هُوَ الْمَعْبُودُ.
Na Rabb Ndiye Mwenye kuabudiwa
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾
((Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua))[13]
قَالَ ابْنُ كَثِيرٍ (رَحِمَهُ اللهُ): الخَالِقُ لِهَذِهِ الأَشْيَاءَ هُوَ الْمُسْتَحِقُّ لِلْعِبَادَةِ. وَأَنْوَاعُ الْعِبَادَةِ الَّتِي أَمَرَ اللهُ بِهَا مِثْلُ: الإِسْلامِ، وَالإِيمَانِ، وَالإِحْسَانِ، وَمِنْهُ: الدُّعَاءُ، وَالْخَوْفُ، وَالرَّجَاءُ، وَالتَّوَكُّلُ، وَالرَّغْبَةُ، وَالرَّهْبَةُ، وَالْخُشُوعُ، وَالْخَشْيَةُ، وَالإِنَابَةُ، وَالاسْتِعَانَةُ، وَالاسْتِعَاذَةُ، وَالاسْتِغَاثَةُ، وَالذَّبْحُ، وَالنَّذْرُ، وَغَيْرُ ذَلَكَ مِنْ أَنْوَاعِ الْعِبَادَةِ الَّتِي أَمَرَ اللهُ بِهَا. كُلُّهَا للهِ تَعَالَى.
Ibn Kathiyr (رحمه الله) amesema: “Muumbaji wa vitu hivi Ndiye Anayestahiki kuabudiwa. Na aina za ‘ibaadah ambazo Allaah Ameziamrisha ni mfano: Al-Islaam (Uislamu), Al-Iymaan (Imani), Al-Ihsaan (Ihsani). Miongoni mwazo ni: Ad-Du’aa (du’aa), Al-Khawf (khofu ya kuogopa mtu au adhabu au kitu), Ar-Rajaa (kutarajai), At-Tawakkul (kutawakali kwa Allaah), Ar-Raghbah (shauku, utashi na matumaini ya jambo la kupendwa), Ar-Rahbah (tisho au kuogopa), Al-Khushuu’ (unyenyekevu), Al-Khashyah (khofu kutokana na utukufu wa Allaah nayo inahusiana na elimu), At-Taqwa (uchaji), Al-Inaabah (kurejea kutubu na utiifu), Al-Isti’aanah (kuomba msaada wa mambo ya kidunia au ya Aakhirah), Al-Isti’aadhah (kuomba kinga), Al-Istighaathah (kuomba msaada, kuokolewa, au kufarijiwa jambo au haja wakati wa shida au kuokolewa), Adh-Dhab-hu (kuchinja), An-Nadhru (kuweka nadhiri), na mengineyo ya aina za ‘ibaadah ambazo Allaah Ameziamrisha. Zote ziwe kwa ajili ya Allaah Ta’aalaa.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake:
وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا ﴿١٨﴾
((Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah))[14]
فَمَنْ صَرَفَ مِنْهَا شَيْئًا لِغَيْرِ اللهِ؛ فَهُوَ مُشْرِكٌ كَافِرٌ.
Basi atakayeelekeza chochote katika hizo (‘ibaadah) kwa asiyekuwa Allaah, basi yeye ni mshirikina, kafiri.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾
((Na yeyote yule anayeomba du’aa (au kuabudu) pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri))[15]
وَفِي الْحَدِيثِ: ((الدُّعَاءُ مخ الْعِبَادَة))
Na katika Hadiyth: ((Du’aa ni ubongo wa ‘Ibaadah))
[Hadiyth hii ni dhaifu. Ameipokea At-Tirmidhiy - Taz Al-Mishkaat (2331). Lakini ipo Hadiyth kama hiyo ambayo ni sahihi isemayo ((Du’aa ni ‘Ibaadah)) Taz. Swahiyh Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr (3407)]
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ ﴿٦٠﴾
((Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingika Jahanam wadhalilike))[16]
وَدَلِيلُ الْخَوْفِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Khawf (kukhofu) ni kauli Yake Ta’aalaa:
فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧٥﴾
((Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini))[17]
وَدَلِيلُ الرَّجَاءِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Ar-Rajaa (kutaraji) ni kauli Yake Ta’aalaa:
فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾
((Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende ‘amali njema na wala asishirikishe yeyote katika ‘ibaadah za Rabb wake”))[18]
وَدَلِيلُ التَّوَكُلِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya At-Tawakkul (kutawakali, kutegemea) kauli Yake Ta’aalaa:
وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣﴾
((Na kwa Allaah Pekee tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini))[19]
وقوله:
Na kauli Yake:
وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ
((Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza))[20]
وَدَلِيلُ الرَّغْبَةِ، وَالرَّهْبَةِ، وَالْخُشُوعِ، قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Ar-Raghbah (shauku, utashi na matumaini ya jambo la kupendwa) na Ar-Rahbah (tisho au kuogopa) na Al-Khushuu’ (unyenyekevu) ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾
((Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea))[21]
وَدَلِيلُ الْخَشْيَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Khashyah (khofu kutokana na utukufu wa Allaah nayo inahusiana na elimu), ni kauli Yake Ta’aalaa:
فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي
((Basi msiwaogope bali Niogopeni))[22]
وَدَلِيلُ الإِنَابَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Inaabah (kurejea kutubu na utiifu) ni kauli Yake:
وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ
((Na rudini kila mara kutubu kwa Rabb wenu na jisalimisheni Kwake))[23]
وَدَلِيلُ الاسْتِعَانَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Isti’aanah (kuomba msaada wa mambo ya kidunia au ya Aakhirah) ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾
((Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada))[24]
وَفِي الْحَدِيثِ: ((...وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللهِ))
Na katika Hadiyth: ((Ukitaka kuomba msaada, basi mwombe Allaah))[25]
وَدَلِيلُ الاسْتِعَاذَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Isti’aadhah (kuomba kinga) ni kauli Yake Ta’aalaa:
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
((Sema: “Najikinga na Rabb wa mapambazuko))[26] na ((Sema: “Najikinga na Rabb wa watu))[27]
وَدَلِيلُ الاسْتِغَاثَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Istighaathah (kuomba msaada, kuokolewa, au kufarijiwa jambo au haja wakati wa shida au kuokolewa), ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ
((Na (kumbukeni) pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni))[28]
وَدَلِيلُ الذَّبْحِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Adh-Dhab-h (kuchinja) kauli Yake Ta’aalaa:
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾
((Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza)) [29]
وَمِنَ السُنَّةِ: ((لعَنَ اللهُ مَنْ ذَبَحَ لِغَيْرِ اللهِ))
Na katika Sunnah: ((Allaah Amemlaani aliyechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah)).[30]
وَدَلِيلُ النَّذْرِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya An-Nadhr (nadhiri) kauli Yake Ta’aalaa:
يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا ﴿٧﴾
(((Ambao) Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana))[31]
الأَصْلُ الثَّانِي: مَعْرِفَةُ دِينِ الإِسْلامِ بِالأَدِلَّةِ.
Msingi Wa Pili: Kuijua Dini Ya Kiislamu Kwa Dalili
وَهُوَ :الاسْتِسْلامُ للهِ بِالتَّوْحِيدِ، وَالانْقِيَادُ لَهُ بِالطَّاعَةِ، وَالْبَرَاءَةُ مِنَ الشِّرْكِ وَأَهْلِهِ، وَهُوَ ثَلاثُ مَرَاتِبَ: الإسْلامُ، وَالإِيمَانُ، وَالإِحْسَانُ. وَكُلُّ مَرْتَبَةٍ لَهَا أَرْكَانٌ.
Nayo ni kujisalimisha kwa Allaah kwa Tawhiyd, na kunyenyekea katika utiifu, na kujiweka mbali na shirki pamoja na watu wake (wa shirki), nao (huo Msingi wa pili) umegawanyika katika daraja tatu; Uislamu, Iymaan, Ihsaan. Na kila daraja ina nguzo.
المرتبة الأولى: الإسلام.
Daraja Ya Kwanza: Uislamu
فَأَرْكَانُ الإِسْلامِ خَمْسَةٌ:
((شَهَادَةُ أَن لا إلٰه إِلا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَإِقَامُ الصَّلاةِ، وَإِيتَاء الزَّكَاةِ، وَصَوْمُ رَمَضَانَ، وَحَجُّ بَيْتِ اللهِ الْحَرَام))
Na nguzo za Kiislamu ni tano:
((Kushuhudia kwa kukiri kwa moyo na kutamka kwamba laa ilaaha illa-Allaah - hakuna Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kufunga Swawm Ramadhwaan, na kuhiji Nyumba Tukufu ya Allaah))[32]
فَدَلِيلُ الشَّهَادَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Shahada ni kauli Yake Ta’aalaa:
شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾
((Allaah Ameshuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye; na Malaika, na wenye elimu (wameshuhudia kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote))[33]
وَمَعْنَاهَا :لا مَعْبُودَ بِحَقٍّ إلا اللهُ، وَحَدُّ النَّفْيِ مِنْ الإِثْبَاتِ ((لَا إِلَـٰهَ)) نَافِيًا جَمِيعَ مَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللهِ ((إلاَّ الله)) مُثْبِتًا الْعِبَادَةَ للهِ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ فِي عِبَادَتِهِ، كَمَا أَنَّهُ لَيْسَ لَهُ شَرِيكٌ فِي مُلْكِهِ.
Na maana yake ni: Hakuna Muabudiwa wa haki ila Allaah Pekee. ((Laa ilaaha – hakuna muabudiwa wa haki)) inakanusha kila kinachoabudiwa pasi na Allaah. Ama ((illa-Allaah – isipokuwa Allaah)) inathibitisha ‘ibaadah zote ni kwa ajili ya Allaah Pekee. Hana mshirika katika ‘ibaadah Zake kama Alivyokuwa hana mshirika katika Ufalme Wake.
وَتَفْسِيرُهَا الَّذِي يُوَضِّحُهَا قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na tafsiri inayobainisha wazi (Shahaadah), ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ ﴿٢٦﴾ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ ﴿٢٧﴾ وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢٨﴾
((Na Ibraahiym alipomwambia baba yake na kaumu yake: “Hakika mimi nimejitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu. “Isipokuwa Ambaye Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoza.” Na akalifanya neno (la ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.))[34]
وقَوْلُهُ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾
((Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislaam tunajisalimisha kwa Allaah.”))[35]
وَدِليلُ شَهَادَةِ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah ni kauli Yake Ta’aalaa:
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٨﴾
((Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini (muongoke) mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah))[36]
وَمَعْنَى شَهَادَة أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ الله: طَاعَتُهُ فِيمَا أَمَرَ، وَتَصْدِيقُهُ فِيمَا أَخْبَرَ، واجْتِنَابُ مَا نَهَى عَنْهُ وَزَجَرَ وأَلا يُعْبَدَ اللهُ إِلا بِمَا شَرَعَ.
Na maana ya kushuhudia kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, ni kumtii yale aliyoyaamrisha, na kumsadikisha katika aliyoyajulisha, na kujiepusha na ambayo ameyakataza na aliyoyatahadharisha, na kwamba Allaah asiabudiwe isipokuwa kwa kufuata yale yaliyowekewa Shariy’ah.
وَدَلِيلُ الصَّلاةِ، وَالزَّكَاةِ، وَتَفْسِيرُ التَّوْحِيدِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Swalaah na Zakaah na tafsiri ya At-Tawhiyd ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾
((Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.))[37]
وَدَلِيلُ الصِّيَامِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Swiyaam ni kauli Yake Ta’aalaa:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾
((Enyi walioamini! Mmeandikiwa shariy’ah ya kufunga Swiyaam kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.))[38]
وَدَلِيلُ الْحَجِّ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Hajj ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾
((Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu.))[39]
الْمَرْتَبَةُ الثَّانِيَةُ: الإِيمَانُ.
Daraja Ya Pili: Iymaan
وَهُوَ:
((بِضْعٌ وَسَبْعُونَ شُعْبَةً، فَأَعْلاهَا قَوْلُ لا إلٰه إِلا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ))
Nayo ni:
((Ina tanzu [matawi] sabiini na kitu. Ya juu yake ni kauli ya “laa ilaaha illa-Allaah” [hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah], na ya chini yake kabisa ni kuondosha uchafu njiani. Na kuona hayaa ni utanzu [tawi] katika tanzu za imani))[40]
وَأَرْكَانُهُ سِتَّةٌ كما فى الحديث:
((أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ))
Na nguzo zake ni sita kama katika Hadiyth:
((Ni kumwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rasuli Wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Al-Qadr [majaaliwa] ya kheri na shari zake)).[41]
وَالدَّلِيلُ عَلَى هَذِهِ الأَرْكَانِ السِّتَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya hizi nguzo sita ni kauli Yake Ta’aalaa:
لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ
((Si wema (pekee) kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi lakini wema (khaswa) ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii))[42]
ودليل القدر قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya Al-Qadr (majaaliwa) ni kauli ya Allaah:
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ﴿٤٩﴾
((Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa makadirio))[43]
الْمَرْتَبَةُ الثَّالِثَةُ: الإِحْسَانُ.
Daraja Ya Tatu: Ihsaan
رُكْنٌ وَاحِدٌ كما فى الحديث: ((أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِن لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ))
Nguzo yake ni moja kama katika Hadiyth: ((Umwabudu Allaah kama kwamba unamuona, na hata kama humuoni, basi Yeye Anakuona))[44]
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ ﴿١٢٨﴾
((Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan.))[45]
وقَوْلُهُ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ ﴿٢١٧﴾ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٢١٨﴾ وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ ﴿٢١٩﴾ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٢٢٠﴾
((Na tawakali kwa Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu. Ambaye Anakuona wakati unaposimama. Na mageuko yako katika wenye kusujudu. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote))[46]
وقَوْلُهُ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ
((Na hushughuliki katika jambo lolote, na wala husomi humo katika Qur-aan, na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo))[47].
وَالدَّلِيلُ مِنَ السُّنَّةِ حَدِيثُ جِبْرِيلَ الْمَشْهُورُ:
Na dalili katika Sunnah ni Hadiyth mashuhuri ya Jibriyl:
عَنْ عُمَرَ بنِ الْخَطَّابِ (رضي الله عنه) قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ النَّبِيِّ (صلى الله عليه وآله وسلم) إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ، شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، فَجَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ (صلى الله عليه وآله وسلم) فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ أَخْبِرْنِي عَنِ الإِسْلامِ فَقَالَ: ((أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلٰه إِلا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَتُقِيمَ الصَّلاةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنْ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلا)) .قَالَ: صَدَقْتَ. فَعَجِبْنَا لَهُ يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ. قَالَ: أَخْبِرْنِي عَنِ الإِيمَانِ. قَال: ((أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ)) قَالَ: صَدَقْتَ. قَالَ: أَخْبِرْنِي عَنِ الإِحْسَانِ. قَال: ((أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ)) قَالَ: أَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ. قَالَ: ((مَا الْمَسْؤُولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ)) .قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَاتِهَا. قَالَ: ((أَنْ تَلِدَ الأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الْحُفَاةَ الْعُرَاةَ الْعَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ فِي الْبُنْيَانِ)) .قَالَ: فَمَضَى، فَلَبِثْنَا مَلِيَّا، فَقَالَ: ((يَا عُمَرُ أَتَدْرُونَ مَنِ السَّائِلِ؟)) قُلْنَا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: ((هَذَا جِبْرِيلُ أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ أَمْرَ دِينِكُم)).
Imepokelewa kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه) amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka magoti yake karibu na magoti yake na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu. Akasema: ((Ni kushuhudia kwa kukiri na kwa moyo kuwa hakuna Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga Swawm Ramadhwaan na kwenda kuhiji [Makkah] ukiweza)) Akasema yule mtu yaani Jibriyl: Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Iymaan. Akasema: ((Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Al-Qadr kheri na shari zake)) Akasema: Umesema kweli. Akasema: Hebu nielezee kuhusu Ihsaan. Akasema: ((Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona na hata kama humuoni basi Yeye Anakuona)). Akasema: Niambie kuhusu Qiyaamah. Akajibu: ((Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile muulizaji)) Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu: ((Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda uchi [wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi], mafukara [wasiokuwa hata na sehemu ya kuishi kwa umaskini] wakishindana kujenga majumba ya fahari.)). Kisha [Jibriyl] akaondoka na nilitulia kidogo [nikitafakari]. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ee 'Umar! Je, mnamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza?)) Nikasema: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Akasema: ((Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha Dini yenu))[48]
الأَصْلُ الثَّالِث: مَعْرِفَةُ نَبِيِّكُمْ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
Msingi Wa Tatu: Kumjua Nabiy Wenu Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)
وَهُوَ مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ بْنِ هَاشِمٍ، وَهَاشِمٌ مِنْ قُرَيْشٍ، وَقُرَيْشٌ مِنَ الْعَرَبِ، وَالْعَرَبُ مِنْ ذُرِّيَّةِ إِسْمَاعِيلَ بْنِ إِبْرَاهِيمَ الْخَلِيلِ عَلَيْهِ وَعَلَى نَبِيِّنَا أَفْضَلُ الصَّلاةِ وَالسَّلامِ، وَلَهُ مِنَ الِعُمُرِ ثَلاثٌ وَسِتُّونَ سَنَةً، مِنْهَا أَرْبَعُونَ قَبْلَ النُّبُوَّةِ، وَثَلاثٌ وَعِشْرُون َفى النبوة. نُبِّئَ ب ((إقْراء)) ، وَأُرْسِلَ ب ((الْمُدَّثِّرْ))، وَبَلَدُهُ مَكَّةُ. بَعَثَهُ اللهُ بِالنِّذَارَةِ عَنِ الشِّرْكِ، وَبالَدْعُوة إِلَى التَّوْحِيدِ.
Naye ni Muhammad bin ‘Abdillaah bin ‘Abdil-Muttwalib bin Haashim. Na Haashim ni kutoka katika (kabila la) la Quraysh. Na Quraysh ni katika Waarabu. Na Waarabu ni kutokana na kizazi cha Ismaa’iyl bin Ibraahiym Al-Khaliyl Swalaah na salamu bora kabisa ziwafikie yeye na Nabiy wetu. Naye alikuwa na umri wa miaka sitini na tatu, miongoni mwa miaka hiyo miaka arubaini kabla ya kupewa Unabiy, na miaka ishirini na tatu akiwa katika Unabiy. Akapewa Unabiy kwa: ((Iqraa - Soma)) na akatumwa (kulingania) kwa ((Al-Muddath-thir – mwenye kujigubika)). Na nchi yake ni Makkah. Allaah Amemtuma kuonya kuhusu shirki na kulingania katika Tawhiyd.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ ﴿١﴾ قُمْ فَأَنذِرْ ﴿٢﴾ وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ ﴿٣﴾ وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ ﴿٤﴾ وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ ﴿٥﴾ وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ ﴿٦﴾ وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ ﴿٧﴾
((Ee mwenye kujigubika! Simama na uonye. Na Rabb wako mtukuze. Na nguo zako toharisha. Na najisi (masanamu) epukana nayo. Na wala usifanye fadhila kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa. Na kwa ajili ya Rabb wako subiri))[49]
وَمَعْنَى قُمْ فَأَنذِرْ ﴿٢﴾ يُنْذِرُ عَنِ الشِّرْكِ، وَيَدْعُو إِلَى التَّوْحِيدِ.
Na maana ya ((Simama na uonye)): Aonye kuhusu shirki na alinganie katika Tawhiyd.
وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ ﴿٣﴾ أَيْ: عَظِّمْهُ بِالتَّوْحِيدِ.
((Na Rabb wako mtukuze)) Yaani: Muadhimishe kwa Tawhiyd.
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ ﴿٤﴾ أَيْ: طَهِّرْ أَعْمَالَكَ عَنِ الشِّرْكِ.
((Na nguo zako toharisha) Yaani: Toharisha ‘amali zako kutokana na shirk.
وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ ﴿٥﴾ الرُّجْزَ: الأَصْنَامُ، وَهَجْرُهَا: تَرْكُهَا، وَالْبَرَاءَةُ مِنْهَا وَأَهْلُهَا.
((Na najisi (masanamu) epukana nayo) Uchafu au najsi ni masanamu. Na kuyahama ni kuepukana nayo kabisa na kujiweka mbali nayo na watu wake.
أَخَذَ عَلَى هَذَا عَشْرَ سِنِينَ يَدْعُو إِلَى التَّوْحِيدِ، وَبَعْدَ الْعَشْرِ عُرِجَ بِهِ إِلَى السَّمَاءِ، وَفُرِضَتْ عَلَيْهِ الصَّلَواتُ الْخَمْسُ، وَصَلَّى فِي مَكَّةَ ثَلاثَ سِنِينَ، وَبَعْدَهَا أُمِرَ بالْهِجْرَةِ إِلَى الْمَدِينَةِ، وَالْهِجْرَةُ الانْتِقَالُ مِنْ بَلَدِ الشِّرْكِ إِلَى بَلَدِ الإِسْلامِ.
Amesimamia haya miaka kumi akilingania katika Tawhiyd. Na baada ya miaka kumi, alipandishwa mbinguni (Mi’iraaj) na akafaridhishwa Swalaah tano, akaswali Makkah miaka mitatu, na baada ya hapo akaamrishwa kuhajiri kwenda Madiynah. Na hijrah ni kuhama kutoka nchi ya shirki kwenda katika nchi ya Kiislamu.
وَالْهِجْرَةُ فَرِيضَةٌ عَلَى هَذِهِ الأُمَّةِ مِنْ بَلَدِ الشِّرْكِ إِلَى بلد الإِسْلامِ، وَهِيَ بَاقِيَةٌ إِلَى أَنْ تَقُومَ السَّاعَةُ.
Na hijrah ni fardhi kwa Ummah huu kuhama kutoka katika nchi ya shirki kwenda nchi ya Kiislamu. Nayo itaendelea kubakia hadi itakaposimama Saa (Qiyaamah).
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾ إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾ فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٩٩﴾
((Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao; (Malaika) watawaambia: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.” (Malaika) Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata (mpango wa) hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao asaa Allaah Akawasamehe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria))[50]
وَقَوْلُهُ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
((“Enyi waja Wangu walioamini! Hakika ardhi Yangu ni pana, basi Mimi Pekee Niabuduni.”))[51]
قَالَ الْبُغَوِيُّ (رَحِمَهُ اللهُ) :نزلت هَذِهِ الآيَةِ فِي المُسْلِمِينَ الَّذِينَ بِمَكَّةَ ولَمْ يُهَاجِرُوا، نَادَاهُمُ اللهُ بِاسْمِ الإِيمَانِ.
Amesema Al-Baghaawiy (رحمه الله): “Aayah hii imeteremshwa kwa sababu ya Waislamu waliokuwa Makkah ambao hawakuhajiri. Allaah Amewaita kwa jina la Waumini.
وَالدَّلِيلُ عَلَى الْهِجْرَةِ مِنَ السُّنَّةِ، قَوْلُهُ (صلى الله عليه وآله وسلم):
((لاَ تَنْقَطِعُ الْهِجْرَةُ حَتَّى تَنْقَطِعَ التَّوْبَةُ، وَلا تَنْقَطِعُ التَّوْبَةُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَ))
Na dalili ya Hijrah (kuhajiri) katika Sunnah ni kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم):
((Hijrah haikatiki mpaka ikatike tawbah. Na tawbah haikatiki mpaka jua lichomoze kutoka Magharibi))[52]
فَلَمَّا اسْتَقَرَّ فِي الْمَدِينَةِ أُمِرَ بِبَقِيَّةِ شَرَائِعِ الإِسْلامِ، مِثلِ: الزَّكَاةِ، وَالصَّوْمِ، وَالْحَجِّ، وَالأَذَانِ، وَالْجِهَادِ، وَالأَمْرِ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّهْيِ عَنِ الْمُنْكَرِ، وَغَيْرِ ذَلِكَ مِنْ شَرَائِعِ الإِسْلامِ، أَخَذَ عَلَى هَذَا عَشْرَ سِنِينَ، وَتُوُفِّيَ ـ صَلواتُ اللهِ وَسَلامُهُ عَلَيْهِ ـ وَدِينُهُ بَاقٍ. وَهَذَا دِينُهُ، لا خَيْرَ إِلا دَلَّ الأُمَّةَ عَلَيْهِ، وَلا شَرَّ إِلا حَذَّرَهَا مِنْهُ، وَالْخَيْرُ الَّذِي دَلَّهَا عَلَيْهِ التَّوْحِيدُ، وَجَمِيعُ مَا يُحِبُّهُ اللهُ وَيَرْضَاهُ، وَالشَّرُ الَّذِي حَذَّرَهَا مِنْهُ الشِّرْكُ، وَجَمِيعُ مَا يَكْرَهُ اللهُ وَيَأْبَاهُ. بَعَثَهُ اللهُ إِلَى النَّاسِ كَافَّةً، وَافْتَرَضَ طَاعَتَهُ عَلَى جَمِيعِ الثَّقَلَيْنِ الْجِنِّ وَالإِنْسِ.
Baada ya kustakiri Madiynah aliamrisha Shariy’ah za Kiislamu zilobakia kama; Zakaah, Swawm, Hajj, Adhaan, Jihaad, kuamrisha mema na kukataza munkari na mengineyo ya Shariy’ah ya Kiislamu. Amefanya hayo miaka kumi akafariki baada ya hapo, Swalaah na salamu ziwe juu yake. Na Dini yake imebaki. Na hii Dini yake, hakuna kheri isipokuwa kawaelekeza kwayo Ummah, na hakuna shari ila amewatahadharisha nayo. Na kheri aliyowaongoza kwayo ni Tawhiyd na yote Anayoyapenda Allaah na Anayoyaridhia. Na shari ambazo amezitahadharisha ni shirki na yote yanayomchukiza Allaah na Asiyoyaridhia. Allaah Amemtuma kwa watu wote, na Amefaradhisha Ath-Thaqalayn (walimwengu wawili); majini na watu kumtii yeye (Nabiy).
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا
((Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote.))[53]
وَكَمَّلَ اللهُ بِهِ الدِّينَ؛ وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na Allaah Ameikamilisha Dini hii kwa kupitia kwake. Na dalili ni kauli ya Yake Ta’aalaa:
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ
((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislaam uwe Dini yenu.))[54]
وَالدَّلِيلُ عَلَى مَوْتِهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ)) قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ya kifo chake (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ﴿٣٠﴾ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ ﴿٣١﴾
((Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) utakufa nao pia watakufa. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyaamah mtakhasimiana mbele ya Rabb wenu.))[55]
وَالنَّاسُ إِذَا مَاتُواْ يُبْعَثُونَ.
Na watu watakapokufa watafufuliwa.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ ﴿٥٥﴾
((Kutokana nayo (ardhi) Tumekuumbeni, na humo Tutakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine))[56]
وقَوْلُهُ تَعَالَى:
Na kauli Yake Ta’aalaa:
وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا ﴿١٧﴾ ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا ﴿١٨﴾
((Na Allaah Amekuanzisheni vizuri katika (udongo wa) ardhi. Kisha Atakurudisheni humo na Atakutoeni tena mtoke (kuwa hai)) [57]
وَبَعْدَ الْبَعْثِ مُحَاسَبُونَ وَمَجْزِيُّونَ بِأَعْمَالِهِمْ.
Na baada ya kufufuliwa watahesabiwa na watalipwa kwa ‘amali zao.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalil ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى ﴿٣١﴾
((Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini ili Awalipe wale waliofanya uovu kwa yale waliyoyatenda, na Awalipe wale waliofanya mema kwa mema zaidi))[58]
وَمَنْ كَذَّبَ بِالْبَعْثِ كَفَرَ.
Na anayekadhibisha kufufuliwa amekufuru.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧﴾
((Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: Bali hapana! Naapa kwa Rabb wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.))[59]
وَأَرْسَلَ اللهُ جَمِيعَ الرُّسُلِ مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ.
Na Allaah Ametuma Rasuli wote wakiwa ni wabashiriaji na waonyaji.
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ
((Rasuli ni wabashiriajina waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rasuli))[60]
وَأَّولُهُمْ نُوحٌ (عَلَيْهِ السَّلامُ)، وَآخِرُهُمْ مُحَمَّدٌ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) وَهُوَ خَاتَمُ النَّبِيِّينَ.
Na wa kwanza wao ni Nuwh (عليه السلام) na wa mwisho wao ni Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) naye ndiye Nabiy wa mwisho.
وَالدَّلِيلُ عَلَى أَنَّ أَوَّلَهُمْ نُوحٌ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili kwamba Nuuh ndio wa mwanzo wao ni kauli Yake Ta’aalaa:
إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ
((Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Nabiy baada yake))[61]
وَكُلُّ أُمَّةٍ بَعَثَ اللهُ إِلَيْهِا رَسُولا مِنْ نُوحٍ إِلَى مُحَمَّدٍ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) يَأْمُرُهُمْ بِعِبَادَةِ اللهِ وَحْدَهُ، وَيَنْهَاهُمْ عَنْ عِبَادَةِ الطَّاغُوتِ.
Na kila Ummah Allaah Ameupelekea Rasuli kuanzia Nuwh hadi kwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Akiwaamrisha kumwabudu Allaah Pekee, na Akiwakataza kuabudu twaghuti[62]
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ
((Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na taghuti))[63].
وَافْتَرَضَ اللهُ عَلَى جَمِيعِ الْعِبَادِ الْكُفْرَ بِالطَّاغُوتِ وَالإِيمَانَ بِاللهِ.
Na Allaah Akafaridhisha kwa waja wote wakanushe twaghuti na kumwamini Allaah (wamwabudu Yeye Pekee).
قَالَ ابْنُ الْقَيِّمِ (رَحِمَهُ اللهُ): مَعْنَى الطَّاغُوتِ مَا تَجَاوَزَ بِهِ الْعَبْدُ حَدَّهُ مِنْ مَعْبُودٍ أَوْ مَتْبُوعٍ أَوْ مُطَاعٍ. وَالطَّوَاغِيتُ كَثِيرُونَ وَرُؤُوسُهُمْ خَمْسَةٌ: إِبْلِيسُ لَعَنَهُ اللهُ، وَمَنْ عُبِدَ وَهُوَ رَاضٍ، وَمَنْ دَعَا النَّاسَ إِلَى عِبَادَةِ نَفْسِهِ، وَمَنْ ادَّعَى شَيْئًا مِنْ عِلْمِ الْغَيْبِ، وَمَنْ حَكَمَ بِغَيْرِ مَا أَنْزَلَ اللهُ.
Ibnul Qayyim (رحمه الله) amesema: “Maana ya twaghuti ni kila anachopindukia mja mipaka yake; ikiwa ni kinachoabudiwa, au kinachofuatwa au kinachotiiwa. Na matwaghuti ni wengi. Wakuu wao ni watano; Ibliys laana za Allaah ziwe juu yake, na anayeabudiwa hali ya kuwa yeye yuko radhi, na anayeita watu wamwabudu yeye, na anayedai kujua elimu ya ghayb (isiyoonekana na kujulikana isipokuwa na Allaah), na anayehukumu yale ambayo Hakuyateremsha Allaah.”
وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى:
Na dalili ni kauli Yake Ta’aalaa:
لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾
((Hapana kulazimisha katika (kuingia) Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaaghuwt (miungu ya uongo) na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote))[64]
وَهَذَا هُوَ مَعْنَى لا إلٰه إِلا اللهُ.
Na hii ndio maana ya Laa ilaaha illa-Allaah (hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah).
وَفِي الْحَدِيث: ((رَأْسُ الأَمْرِ الإِسْلامِ، وَعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ))
Na katika Hadiyth: ((Msingi wa mambo ni Uislamu, na nguzo yake ni Swalaah na kilele cha nundu yake ni kupigana katika njia ya Allaah))[65]
وَاللهُ أَعْلَمُ. وَصَلَّى اللهُ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعلى آلٰه وَصَحْبِهِ وَسَلَّمَ.
Na Allaah Anajua zaidi wa Swalla Allaahu ‘alaa Muhammadi wa ‘alaa aalihi wa Swahabihi wa sallam.
[1]Marejeo: Imaam Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab Da’watuhuu wa Siyraatuhu - Shaykh Ibn Baaz.
[2] Al-‘Aswr (103).
[3] Muhammad (47: 19).
[4] Al-Muz-zzammil (73: 15-16).
[5] Al-Jinn (72: 18).
[6] Al-Mujaadilah (58: 22).
[7] Adh-Dhaariyaat (51: 56).
[8] An-Nisaa (4: 36).
[9] Al-Faatihah: (1: 2).
[10] Fusswilat (41: 37).
[11] Faida: Maana ya Istawaa: Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah. Pia rejea tanbih (2: 29).
[12] Al-A’raaf (7: 54).
[13] Al-Baqarah (2: 21-22).
[14] Al-Jinn (72: 18).
[15] Al-Muuminuwn (23: 117).
[16] Ghaafir (40: 60).
[17] Aal-’Imraan (3: 175).
[18] Al-Kahf (18: 110).
[19] Al-Maaidah (5: 23).
[20] Atw-Twalaaq (65: 3).
[21] Al-Anbiyaa (21: 90).
[22] Al-Baqarah (2: 150).
[23] Az-Zumar (39: 54).
[24] Al-Faatihah (1: 5).
[25] At-Tirmidhiy ni Hadiyth Swahiyh kama alivyothibitisha Al-Albaaniy.
[26] Al-Falaq (113: 1).
[27] An-Naas (114: 1).
[28] Al-Anfaal (8: 9).
[29] Al-An’aam (6: 161-163).
[30] Muslim.
[31] Al-Insaan (76: 7).
[32] Muslim.
[33] Aal-‘Imraan (3: 18).
[34] Az-Zukhruf (43: 26-28).
[35] Aal-‘Imraan (3: 64).
[36] At-Tawbah (9: 128).
[37] Al-Bayyinah (98: 5).
[38] Al-Baqarah (2: 183).
[39] Aal-‘Imraan (3: 97).
[40] Al-Bukhaariy na Muslim.
[41] Muslim.
[42] Al-Baqarah (2: 177).
[43] Al-Qamar (54: 49).
[44] Muslim -Hadiyth mashuhuri ya kuja Jibrily kumfunza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) mas-alah ya Dini yake.
[45] An-Nahl (16: 128).
[46] Ash-Shu’araa (26: 217-220).
[47] Yuwnus (10: 61).
[48] Muslim.
[49] Al-Muddath-thir (74: 1-7).
[50] An-Nisaa (4: 97-99).
[51] Al-‘Ankabuwt (29: 56).
[52]Abu Daawuwd, Ahmad, Ad-Daarimiy na ni Swahiyh kwa mujibu wa Al-Albaaniy katika Swahiyhul-Jaami’ As-Swaghiyr 7346.
[53] Al-A’raaf (7: 158).
[54] Al-Maaidah (5: 3).
[55] Az-Zumar (39: 30-31).
[56] Twaahaa (20: 55).
[57] Nuuh (71: 17-18).
[58] An-Najm (53: 31).
[59] At-Taghaabun (64: 7).
[60] An-Nisaa (4: 165).
[61] An-Nisaa (4: 163).
[62] Miungu yote ya uongo na vyote viabudiwavyo kwa batili kama mashetani, masanamu, mizimu, watu n.k.
[63] An-Nahl (16: 36).
[64] Al-Baqarah (2: 256).
[65] At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na ni Swahiyh kwa mujibu wa Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-Tirmidhiy (2110)