046 - Al-Ahqaaf
الأَحْقَاف
046-Al-Ahqaaf
046-Al-Ahqaaf: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
مَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ﴿٣﴾
3. Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na kwa muda maalumu uliokadiriwa. Na waliokufuru wanayakengeuka yale wanayoonywa.
قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ ۖ ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِّن قَبْلِ هَـٰذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِّنْ عِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٤﴾
4. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnawaona wale mnaowaomba badala ya Allaah! Nionyesheni nini wameumba katika ardhi, au wana ushirika katika mbingu?[2] Nileteeni Kitabu kabla ya hiki, au alama yeyote ya ilimu mkiwa wakweli.
وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾
5. Na nani aliyepotoka zaidi kuliko yule anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah? Nao wala hawatambui maombi yao!
وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ﴿٦﴾
6. Na pale watakapokusanywa watu, (waabudiwa wa uongo) watakuwa ni maadui wao, na watakuwa wenye kuzikanusha ibaada zao.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧﴾
7. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, husema wale waliokufuru kuhusu haki ilipowajia: Hii ni sihiri bayana.[3]
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَلَا تَمْلِكُونَ لِي مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِ ۖ كَفَىٰ بِهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۖ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٨﴾
8. Bali wanasema ameitunga. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ikiwa nimeitunga, basi hamna uwezo wa kunifaa chochote mbele ya Allaah. Yeye Anajua zaidi yale mnayoyaropoka. Anatosha kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu, Naye Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[4]
قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٩﴾
9. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mimi sio wa mwanzo kuja na Urasuli (Utume) miongoni mwa Rusuli, na sijui nitakavyofanyiwa mimi wala nyinyi.[5] Sifuati isipokuwa niliyofunuliwa Wahy, nami si chochote isipokuwa ni mwonyaji bayana.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَكَفَرْتُم بِهِ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِ فَآمَنَ وَاسْتَكْبَرْتُمْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠﴾
10. Sema: Mnaonaje ikiwa (hii Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, na mkaikanusha, na akashuhudia shahidi miongoni mwa wana wa Israaiyl juu ya mfano wa haya, na akaamini nanyi mkatabari? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.[6]
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا لَوْ كَانَ خَيْرًا مَّا سَبَقُونَا إِلَيْهِ ۚ وَإِذْ لَمْ يَهْتَدُوا بِهِ فَسَيَقُولُونَ هَـٰذَا إِفْكٌ قَدِيمٌ﴿١١﴾
11. Na wale waliokufuru wakasema kuwaambia walioamini: Lau ingelikuwa ni kheri, basi wasingetusabiki. Na kwa kuwa hawakuhidika kwayo (Qur-aan), basi watasema: Huu ni uzushi wa zamani.
وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ وَهَـٰذَا كِتَابٌ مُّصَدِّقٌ لِّسَانًا عَرَبِيًّا لِّيُنذِرَ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَبُشْرَىٰ لِلْمُحْسِنِينَ﴿١٢﴾
12. Na kabla yake ni kitabu cha Muwsaa chenye kuongoza, na kuwa ni rehma. Na hiki Kitabu kinasadikisha kwa lugha ya Kiarabu ili kionye wale waliodhulumu, na ni bishara kwa wafanyao ihsaan.
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿١٣﴾
13. Hakika wale waliosema: Rabb wetu ni Allaah, kisha wakathibiti imara, basi hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.[7]
أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٤﴾
14. Hao ndio watu wa Jannah, ni wenye kudumu humo, jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿١٥﴾
15. Na Tumemuusia binaadam kuwafanyia wema wazazi wake wawili.[8] Mama yake amebeba mimba yake kwa mashaka na akamzaa kwa mashaka.[9] Na kuibeba mimba na kuachishwa kwake kunyonya ni miezi thelathini.[10] Mpaka anapofikia umri wake wa kupevuka, na akafikia miaka arubaini husema: Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Nitengenezee dhuria wangu. Hakika mimi nimetubu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu.[11]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ نَتَقَبَّلُ عَنْهُمْ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَنَتَجَاوَزُ عَن سَيِّئَاتِهِمْ فِي أَصْحَابِ الْجَنَّةِ ۖ وَعْدَ الصِّدْقِ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ﴿١٦﴾
16. Hao ndio wale ambao Tunawatakabalia mazuri zaidi ya yale waliyoyatenda, na Tunayaachilia mbali maovu yao, watakuwa katika watu wa Jannah. Ahadi ya kweli waliyokuwa wameahidiwa.
وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَّكُمَا أَتَعِدَانِنِي أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ الْقُرُونُ مِن قَبْلِي وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ اللَّـهَ وَيْلَكَ آمِنْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٧﴾
17. Na yule anaewaambia wazazi wake: Uff![12] Mnanitishia kwamba nitatolewa kufufuliwa na hali zimekwishapita karne nyingi kabla yangu! Nao wazazi wawili wanaomba uokozi kwa Allaah, na (humwambia mtoto wao): Ole wako amini! Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Lakini husema: Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.[13]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ﴿١٨﴾
18. Hao ndio wale ambao imehakiki juu yao kauli (ya adhabu) kama katika nyumati nyingi zilizokwishapita kabla yao miongoni mwa majini na wanaadam. Hakika wao wamekuwa ni wenye kukhasirika.
وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۖ وَلِيُوَفِّيَهُمْ أَعْمَالَهُمْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١٩﴾
19. Na wote watakuwa na daraja mbali mbali kutokana na yale waliyoyatenda, na ili (Allaah) Awalipe kikamilifu amali zao, nao hawatodhulumiwa.
وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَاتِكُمْ فِي حَيَاتِكُمُ الدُّنْيَا وَاسْتَمْتَعْتُم بِهَا فَالْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَفْسُقُونَ﴿٢٠﴾
20. Na siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (waambiwe): Je, mshamaliza vizuri vyenu katika uhai wenu wa dunia na mshajistarehesha navyo? Basi leo mtalipwa adhabu ya udhalilifu kwa vile mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa ufasiki mliokuwa mnaufanya.
وَاذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنذَرَ قَوْمَهُ بِالْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ النُّذُرُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴿٢١﴾
21. Na mtaje (Huwd) ndugu wa kina ‘Aad alipowaonya watu wake katika nchi ya machuguu ya mchanga,[14] na walikwishapita waonyaji kabla yake na baada yake: Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَأْفِكَنَا عَنْ آلِهَتِنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٢٢﴾
22. Wakasema: Je, umetujia ili utugeuzilie mbali na waabudiwa wetu? Basi tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَأُبَلِّغُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ﴿٢٣﴾
23. (Huwd) akasema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah, nami nabalighisha ambayo nimetumwa kwayo, lakini nakuoneni nyinyi ni kaumu wenye kufanya ujahili.
فَلَمَّا رَأَوْهُ عَارِضًا مُّسْتَقْبِلَ أَوْدِيَتِهِمْ قَالُوا هَـٰذَا عَارِضٌ مُّمْطِرُنَا ۚ بَلْ هُوَ مَا اسْتَعْجَلْتُم بِهِ ۖ رِيحٌ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢٤﴾
24. Basi walipoiona (adhabu waliyoihimiza) ni wingu lilotanda upeoni (mwao) linaelekea mabonde yao walisema: Wingu hili lilotanda upeoni (mwetu) ni la kutunyeshea mvua. Bali hilo ndilo mloharakiza, ni upepo wa dhoruba ndani yake kuna adhabu iumizayo.
تُدَمِّرُ كُلَّ شَيْءٍ بِأَمْرِ رَبِّهَا فَأَصْبَحُوا لَا يُرَىٰ إِلَّا مَسَاكِنُهُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴿٢٥﴾
25. Unadamirisha kila kitu kwa Amri ya Rabb wake. Wakapambaukiwa hayaonekani isipokuwa masikani zao tu. Hivyo ndivyo Tunavyolipa jazaa watu wahalifu.
وَلَقَدْ مَكَّنَّاهُمْ فِيمَا إِن مَّكَّنَّاكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَارًا وَأَفْئِدَةً فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَا أَبْصَارُهُمْ وَلَا أَفْئِدَتُهُم مِّن شَيْءٍ إِذْ كَانُوا يَجْحَدُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٢٦﴾
26. Na kwa yakini Tuliwamakinisha vizuri zaidi kuliko Tulivyokumakinisheni (nyinyi Maquraysh). Na Tukawapa masikio na macho na nyoyo za kutafakari, lakini hayakuwafaa chochote masikio yao wala macho yao wala nyoyo zao za kutafakari kwa kuwa walikuwa wakikanusha kwa ujeuri Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) za Allaah, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا مَا حَوْلَكُم مِّنَ الْقُرَىٰ وَصَرَّفْنَا الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٧﴾
27. Na kwa yakini Tuliangamiza miji iliyokuwa pembezoni mwenu, na Tukasarifu waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) ili wapate kurejea.
فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ قُرْبَانًا آلِهَةً ۖ بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٢٨﴾
28. Basi kwa nini wasiwanusuru wale waliowafanya badala ya Allaah kuwa ni waabudiwa wa kikurubisho (Kwake)? Bali wamewapotea, na huo ndio uongo wao na yale waliyokuwa wakiyatunga.
وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ﴿٢٩﴾
29. Na pale Tulipowaelekeza kwako (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم ) kundi miongoni mwa majini ili kuisikiliza Qur-aan. Walipohudhuria majlisi, walisema: Bakieni kimya msikilize! Ilipomalizika, waligeuka kurudi kwa kaumu yao wakiwa wenye kuonya.[15]
قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٣٠﴾
30. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kimeteremshwa baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka.
يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣١﴾
31. Enyi kaumu yetu! Mwitikieni Mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini! (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo.
وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّـهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءُ ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٢﴾
32. Na yeyote asiyemuitikia Mlinganiaji wa Allaah, basi hawezi kushinda kukwepa katika ardhi, na hatokuwa na walinzi badala ya Allaah. Hao wamo katika upotofu bayana.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ۚ بَلَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٣﴾
33. Je, hawaoni kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na wala Hakuchoka kwa kuziumba kwake, kwamba Yeye Ni Muweza wa Kuwafufua wafu. Naam bila shaka! Hakika Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.[16]
وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ﴿٣٤﴾
34. Na Siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (isemwe): Je, hii si kweli? Watasema: Bali ndio! Tunaapa kwa Rabb wetu! Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri mliokuwa mkiufanya.
فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِل لَّهُمْ ۚ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّن نَّهَارٍ ۚ بَلَاغٌ ۚ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ﴿٣٥﴾
35. Basi subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama walivyosubiri wenye azimio madhubuti miongoni mwa Rusuli[17], na wala usiwaharakizie. Siku watakayoona waliyoahidiwa itakuwa kama kwamba hawakubakia (duniani) isipokuwa saa moja tu katika mchana. (Huu) ni ubalighisho! Je, basi kwani huangamizwa isipokuwa watu mafasiki?
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Wanaoabudiwa Pasi Na Allaah Hawakuumba Chochote:
Rejea Luqmaan (31:11) kwenye rejea mbali mbali.
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى)
أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ
Au wana ushirika katika mbingu.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaraddi kwa hili kwamba ingelikuwa wana ushirika Naye katika Uumbaji Wake mbingu na ardhi, basi kila mwabudiwa angelichukua vile alivyoviumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Rejea Al-Muuminuwn (23:91). Au pia mbingu na ardhi bila shaka zingelifisidika. Rejea Al-Anbiyaa (21:22).
Bali Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mshirika na Ndiye Aliyeumba kila kitu. Rejea Al-An’aam (6:101-102), Az-Zumar (39:62).
[3] Ada Ya Makafiri Kuipachika Sifa Ovu Qur-aan:
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa hayo na rejea mbalimbali.
[4] Washirikina Kumsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuwa Ameitunga Qur-aan:
Au je wanasema hawa washirikina kwamba Muhammad ametunga Quraan? Waambie, ee Rasuli! “Iwapo mimi nimemtungia Allaah hii Qur-aan, basi nyinyi hamuwezi kunikinga mimi na Adhabu ya Allaah kwa lolote ikiwa Ataniadhibu kwa hilo. Yeye (سبحانه وتعالى) kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi zaidi wa kile mnachokisema juu ya hii Qur-aan kuliko kitu chochote kingine. Inatosha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Shahidi juu yangu mimi na nyinyi, na Yeye Ndiye Mwingi wa Kughufuria Waja Wake, na Ni Mwingi wa Kuwarehemu Waja Wake Waumini.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni kama Kauli Zake nyenginezo katika Suwrah zifuatazo: Al-Haaqqah (69:44-47), Al-Jinn (71:22-23).
[5] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakuwa Anajua Kama Ataghufuriwa Madhambi Yake:
Amesema ‘Aliy Bin Abiy Twalhah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Baada ya kuteremshiwa Aayah hii, ikateremshwa:
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana. [Al-Fat-h (48:1)]
Na wamesema hayo pia ‘Ikrimah, Al-Hasan na Qataadah kwamba kauli hiyo (ya Suwrah Al-Ahqaaf (46:9) imefutwa hukmu yake kwa kuteremshwa:
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana. [Al-Fat-h (48:1)]
Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwenye Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah:
048-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Fat-h Aayah 01-5: إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا
[6] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/ Shahidi Miongoni Mwa Wana Wa Israaiyl Ni ‘Abdullaah Bin Salaam (رضي الله عنه):
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Na Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) imethibitisha pia:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ سَمِعْتُ مَالِكًا، يُحَدِّثُ عَنْ أَبِي النَّضْرِ، مَوْلَى عُمَرَ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ عَنْ عَامِرِ بْنِ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ مَا سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ لأَحَدٍ يَمْشِي عَلَى الأَرْضِ إِنَّهُ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ. إِلاَّ لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلاَمٍ قَالَ وَفِيهِ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ الآيَةَ. قَالَ لاَ أَدْرِي قَالَ مَالِكٌ الآيَةَ أَوْ فِي الْحَدِيثِ.
Amesimulia Sa’d Bin Abiy Waqqaas kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما):
Sijapata kumsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akimwambia yeyote anayetembea katika ardhi kuwa yeye ni katika watu wa Jannah isipokuwa ‘Abdullaah bin Salaam. Na kwa ajili yake imeteremshwa Aayah hii:
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَكَفَرْتُم بِهِ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِ فَآمَنَ وَاسْتَكْبَرْتُمْ ۖ
Sema: Mnaonaje ikiwa (hii Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, na mkaikanusha, na akashuhudia shahidi miongoni mwa wana wa Israaiyl juu ya mfano wa haya, na akaamini nanyi mkatabari? [Al-Ahqaaf (46:10]
Akasema: Sijui kama Maalik aliisoma Aayah pembeni au Aayah iko ndani ya Hadiyth. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila za Anaswaar (63)]
Sema ee Rasuli uwaambie washirikina wa watu wako: “Hebu nielezeni. Ikiwa Qur-aan hii inatoka kwa Allaah na nyinyi mmeikataa, halafu akashuhudia shahidi kati ya Wana wa Israaiyl kama ‘Abdullaah bin Salaam kwamba yaliyomo ndani ya Tawraat yanathibitisha Unabii wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kama inavyothibitisha Qur-aan, halafu isitoshe, akayasadikisha na kuyafuata kwa kivitendo yaliyokuja ndani ya Qur-aan na nyinyi mkayakataa kwa njia ya kibri, sasa haya yote ni nini kama si dhulma mbaya na ukafiri mkubwa kutoka kwenu?! Hakika Allaah Hawaongozi kwenye Uislamu na kuifikia haki wale watu waliojidhulumu kwa kumkanusha Allaah. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[8] Kuwafanyia Wazazi Ihsaan:
Na Tumemuusia binaadam asuhubiane na wazazi wake wawili kwa ihsaan, kwa kuwatendea wema wanapokuwa hai na baada ya kufa kwao. Kwa kuwa mamake alimbeba akiwa mwana wa matumboni kwa mashaka na tabu, na akamzaa kwa mashaka na tabu pia. Na muda wa kubeba mimba yake na mpaka kumaliza kumnyonyesha ni miezi thelathini. Katika kutaja mashaka haya anayoyabeba mama, na siyo baba, pana dalili kuwa haki yake juu ya mtoto wake ni kubwa zaidi kuliko haki ya baba. Mpaka alipofikia binaadam upeo wa nguvu zake za kimwili na kiakili na akafikia miaka arubaini, huwa akimuomba Rabb wake kwa kusema: Rabb wangu, Nizindushe nishukuru Neema Zako Ulizonineemesha mimi na wazazi wangu wawili, na Nijaalie nifanye matendo mema Unayoridhika nayo, na Unisuluhishie wanangu. Hakika mimi nimetubia dhambi zangu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa wanyenyekevu Kwako kwa utiifu, na ni miongoni mwa wenye kujisalimisha kufuata Amri Zako, na kuepuka Makatazo Yako, na wenye kuridhia Hukmu Yako. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na jambo hili la kuwafanyia wazazi wawili ihsaan, Allaah (سبحانه وتعالى) Amelipa umuhimu mkubwa mno. Anahimiza hivyo katika Kauli Zake kadhaa. Rejea Luqmaan (31:14) kwenye maelezo na faida tele.
Bonyeza pia viungo vifuatavyo upate faida tele nyenginezo:
040-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wazazi na Kuunga Kizazi (Ujamaa)
041-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kuwaasi Wazazi na Kukata Kizazi
[9] Mashaka Ya Mama Kubeba Mimba Kuzaa:
Aayah hii imetaja mashaka ya mama kubeba mimba na kumzaa mtoto kwa mashaka na mashaka. Na katika Suwrah Luqmaan (31:14), imetajwa amebeba mimba na kumzaa kwa udhaifu juu ya udhaifu. Rejea huko kwenye maelezo na faida nyenginezo.
[11] Duaa Ya Kuomba Msaada Wa Kuweza Kumshukuru Allaah (عزّ وجلّ):
Duaa kama hii imekariri katika Suwrah An-Naml (27:19).
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah za mbinguni, ardhini, nafsini na kadhaalika pamoja na faida nyenginezo na rejea mbalimbali.
Rejea pia Adhw-Dhwuhaa (93:11) kwenye faida kuhusu kukiri Neema za Allaah, kushukuru, na kuomba kuhifadhiwa na kuzidishiwa Neema za Allaah (عزّ وجلّ).
[13] ‘Aaishah (رضي الله عنها) Amtetea Kaka Yake Aliyesingiziwa Kuwa Aayaah Hii Imeteremka Kumhusu Yeye:
حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ مَاهَكَ، قَالَ كَانَ مَرْوَانُ عَلَى الْحِجَازِ اسْتَعْمَلَهُ مُعَاوِيَةُ، فَخَطَبَ فَجَعَلَ يَذْكُرُ يَزِيدَ بْنَ مُعَاوِيَةَ، لِكَىْ يُبَايِعَ لَهُ بَعْدَ أَبِيهِ، فَقَالَ لَهُ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ شَيْئًا، فَقَالَ خُذُوهُ. فَدَخَلَ بَيْتَ عَائِشَةَ فَلَمْ يَقْدِرُوا {عَلَيْهِ} فَقَالَ مَرْوَانُ إِنَّ هَذَا الَّذِي أَنْزَلَ اللَّهُ فِيهِ وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَكُمَا أَتَعِدَانِنِي . فَقَالَتْ عَائِشَةُ مِنْ وَرَاءِ الْحِجَابِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ فِينَا شَيْئًا مِنَ الْقُرْآنِ إِلاَّ أَنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ عُذْرِي.
Amesimulia Yuwsuf bin Maahak (رضي الله عنه): Marwaan (رضي الله عنه) aliteuliwa na Mu’aawiyah (رضي الله عنه) kuwa liwali (gavana) wa Hijaaz. Alitoa khutbah na kumtaja Yaziyd bin Mu‘aawiyah ili watu watoe ahadi ya utiifu kwake baada ya babake. ‘Abdur-Rahmaan bin Abi Bakr (رضي الله عنهما) alimwambia kitu, naye Marwaan akaagizia ashikwe (ili afungwe). Hapo ‘Abdur-Rahmaan aliingia katika nyumba ya ‘Aaishah (رضي الله عنها), kwa hiyo hawakuweza kumshika. Hapo Marwaan akasema: Huyu ni yule aliyeteremshiwa Aayah ifuatayo na Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَّكُمَا أَتَعِدَانِنِي أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ الْقُرُونُ مِن قَبْلِي وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ اللَّـهَ وَيْلَكَ آمِنْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٧﴾
Na yule anaewaambia wazazi wake: Uff! Mnanitishia kwamba nitatolewa kufufuliwa na hali zimekwishapita karne nyingi kabla yangu! Nao wazazi wawili wanaomba uokozi kwa Allaah, na (humwambia mtoto wao): Ole wako amini! Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Lakini husema: Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale. [Al-Ahqaaf (46:17)]
‘Aaishah (رضي الله عنها)akasema akiwa nyuma ya pazia: “Allaah Hakuteremsha chochote kutuhusu sisi katika Qur-aan isipokuwa Allaah Ameteremsha kunitakasa mimi na kashfa ya kusingiziwa kuzini.” [Al-Bukhaariy]
[14] Al-Ahqaaf: Nchi Ya Machuguu Ya Mchanga
Kauli za Salaf kuhusu Ahqaaf:
Ibn Zayd amesema: Ni mlima wa mchanga au pango.
‘Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه): Ni bonde lililoko Hadhwramawt linaloitwa Barhuwt ambapo hutupwa ndani yake roho za makafiri.
Qataadah: Tumetajiwa kwamba kina ‘Aad walikuwa ni kabila la watu wa Yemen. Waliishi katika milima ya michanga iliyochomozea baharini katika ardhi iliyojulikana kama Ash-Shihir.
Na mataje ee Rasuli Nabiy wa Allaah, Huwd (عليه السّلام) ndugu yao kina ‘Aad kinasaba na siyo kidini, alipowaonya watu wake kuwa watashukiwa na Adhabu ya Allaah wakiwa kwenye nyumba zao hapo Aḥqaaf (mahali kwenye mchanga mwingi) kusini mwa Arabuni. Na kwa hakika wamepita Rusuli wakawaonya watu wa mahala hapo kabla ya Huwd na baada yake wakiwaambia: “Msimshirikishe Allaah na kitu chochote mnapomuabudu, hakika sisi tunawacheleeni nyinyi adhabu ya Allaah katika Siku yenye kituko kikubwa, nayo ni Siku ya Qiyaamah.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
[15] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho
Majini Wamelingania Dini Kwa Majini Wenzao:
Rejea Al-Jinn (72:1).
[16] Allaah (عزّ وجلّ) Ni Mweza Wa Kuwafufua Wafu:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[17] Rusuli Walioitwa Ulul-‘Azmi (Wenye Azimio La Nguvu):
Ni Rusuli watano ambao ni: (i) Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii) Nabiy Nuwh (عليه السّلام) (iii) Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) (iv) Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) (v) Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Rejea Al-Ahzaab (33:7) walipotajwa na kwenye maelezo yake. Na rejea pia An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo bayana kuhusu daraja za Rusuli kulingana na Manabii.