Imaam Ibn Taymiyyah: Nani Mwenye Akili?
Nani Mwenye Akili?
Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
"Haitwi 'Mwenye Akili' isipokuwa yule mwenye kuijua khayr akaitaka, na akaijua shari akaiacha.
Na kwa hivyo, walisema watu wa Motoni:
وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١٠﴾
Na watasema: “Lau tungelikuwa tunasikiliza au tunatia akilini, tusingelikuwa katika watu wa motoni.” [Al-Mulk: 10]
[Al-Fataawa, juz. 7, uk. 24]
