Deni La Mtu Asiyejulikana Yuko Wapi

 

 

SWALI:

ASSALAM ALAIKUM

NATEGEMEA MWENYEZI MUNGU ANAENDELEA KUKUPENI NGUVU ZA KUWEZA KUTUJIBU MASWALI YETU

MIMI SWALA LANGU. ZAMANI NILIKWENDA DUKANI NA KUNUNUA KITU NA IKAWA BADO PESA KIDOGO HAZIJATIMIA NA MWENYE KUUZA ALINAMBIA KUA NIPE ULICHONACHO KILICHOBAKI UKIPATA UTANILETEA SASA NILIPOKIPATA NIMEMTAFUTA PAHALI NILIPOKUA NIMENUNUA KILE KITU KWAKE SIKUMPATA NA NIMEJARIBU TENA KUMTAFUTA SIKUMUONA SASA VIPI HIZI PESA NAWEZA NIKAZITOA SADAKA AU NIFANYE NINI MAANA NINA WASIWASI NA ZINANIKERA NA SASA HATA NIKIMUONA NITAKUA SIMJUI. VIPI NAOMBA MNISAIDIE.

NA SWALI JENGINE KUNA MTU ALIKWENDA DUKANI NA MTOTO NA PIA PESA ILIOBAKI KWA YULE MTU MWENYE DUKA ALIMWAMBIA KUA UKIZIPATA NILETEE SASA ALIPOFIKA KWAO ALISEMA MWENYE DUKA AMESEMA ZILIZOBAKI ZIPELEKWE NA HUYU MTOTO ANAPAJUA NI WAPI LAKINI ZILIPOPATIKANA ZINATAKA KUPELEKWA HUYO MTOTO MDOGO ANAULIZWA NI WAPI ANASEMA KUWA HAPAJUI TENA NA HUYO MTU ALIEACHA HAYO MAAGIZO KESHAKUFA NA HIZI PESA BADO ZINAWAKERA SASA WAFANYE NINI SHEIKH

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tunamshukuru Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa neema chungu mzima ambazo Ametupatia sisi kama wanaadamu na hasa kama Waislamu. Tunashukuru kwa swali hili kuhusu mkopo. Kwa hakika tunampongeza dada yetu kwa kuwa na Imani ya kutaka kuona kuwa amelipa deni analodaiwa kabla ya kufariki. Kwa hakika deni halisamehewi mpaka lilipwe au anayekudai akusamehe. Na ilikuwa ada ya Mtume wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutomswalia mtu yeyote mpaka ahakikishe kuwa hana deni au akiwa nalo basi jamaa yake achukue ahadi ya kulilipa.

Na juhudi zako zinaonyesha kuwa una hamu kubwa ya kukamilisha madeni ya wanaadamu hapa hapa duniani. La kutambua ni kuwa Allah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri iwezavyo.

 ((Mwenyezi Mungu Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo))

(2: 286)  

Nawe umejaribu njia zote kuweza kumpata lakini bila ya mafanikio.

Inavyokupasa kufanya sasa ni moja katika yafuatayo:

1) Kuziweka hizo hela na lau atakuja mtu kukwambia kuwa anakudai basi umwamini na umpe ikiwa atataja kiwango ambacho ni sawa na kile unachodaiwa. Na ni vyema katika wasiya wako uandike na uwaachie warithi wako wajue kuwa unadaiwa na mtu hela kadhaa, na atakapotokea wakati ushafariki basi  apatiwe. Ikiwa hajapatikana kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) atakusamehe kwa kuwa umefanya juhudi zako zote za kulipa deni hilo kwa mwenyewe.

      2)  Ukipenda utoe hizo pesa sadaka kwa nia ya huyo mtu kwa sharti kwamba pindi atakapotokea umuelezee ulivyofanya, na ikiwa ataridhika sawa, na kama hakuridhika basi uwe tayari kumlipa wewe pesa zake na muombe Allaah Akutaqabalie zile ulizotoa mwanzo kuwa ziwe  ni sadaka yako.

Kuhusu deni la mwenye duka inawapasa kwanza wazazi wa huyo mtoto wafanye juhudi zote za kumtafuta mwenye duka kwa kuuliza wenye maduka yaliokaribu yao kama yupo mwenye kudai kwa kuelezewa kuhusu mtoto huyo aliyefariki, na kama hakupatikana basi   wazazi wafanye hivyo hivyo kama tulivyoeleza hapo juu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share