Alama Ya Mwezi Katika Misikiti
SWALI:
Nimefurahi
Swali: KWA NINI MISIKITI MINGI IMEWEKEWA ALAMA YA MWEZI? KAMA ALAMA HII NDO INATUMIKA KUASHIRIA MSIKITI,VP ISITUMIKE ALAMA NYINGINE KM JUA, MBINGU, MILIMA N.K. KWA SABABU VYOTE HIVI NI VIUMBE VYA M MUNGU NA NI ISHARA YA KUWEPO KWA ALLAH. SWALI HILI LINANICHANGANYA
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwa hakika alama na ishara hizo hazina umuhimu wala maana yoyote katika kuwekwa katika Misikiti au sehemu nyingine zozote. Kwani wakati wa Mtume (Swalla-Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya-Allaahu 'anhum) alama
Baada ya hapo huenda Waislamu wakaamua kuwa wawe na ishara kama vile Mayahudi na Manaswara, kwani Mayahudi wana ile ishara ya nyota ya Daudi ambayo ina pembe sita na Manaswara wana ishara ya kuwa na msalaba. Kwa kuwa sisi huwa tarehe zetu za siku na miezi yetu hufuata mwezi, basi baadhi ya Waislam wakaona kuwa waweke hiyo alama ya mwezi kama nembo, lakini kiuhakika haina maana yoyote ya kisheria.
Na Allah Anajua zaidi.