Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Kutikisa Kichwa Wakati Wa Kutoa Salaam
Hukmu Ya Kutikisa Kichwa Wakati Wa Kutoa Salaam
Aliulizwa Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah):
Kuna baadhi ya watu, wakati wa kutoa salaam baina ya salaam ya kwanza na salaam ya pili (katikati ya salaam) hutikisa kichwa kuelekea chini; je, ni ipi hukmu ya hilo?
Akajibu kwa kusema:
Jambo hilo halina asili na ni makruhu kufanya hivyo kwani hakuna asili (dalili) juu ya hilo.
[Fataawa Nuurun 'Alaa Ad-Darb, juzuu 9, uk. 29]