Kuvaa Pete Za Vito Ni Shirki?

 

 

Kuvaa Pete Za Vito Ni Shirki?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Kwani leo hii watu asilimia yingi utaona wamevaa pete zenye vinto mbalimbali je ...kuna  shiriki ndani yake hapo au urembo tuh

 

JIBU

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Ikiwa mtu kavaa pete za aina hizo za vito kwa lengo la mapambo tu ni jambo ambalo halijakatazwa lakini pete za aina hizo wengi wanaozivaa ni Mashia au wale waliodanganywa na Mashia. Na Mashia ni maadui wa Uislamu na wako mbali na Uislamu. Haifai kujifananisha na maadui wa Uislamu.

 

Na kuvaa pete si katika Sunnah bali ni jambo ambalo halina makatazo ila ni bora kujiepusha na kujifananisha na Mashia na Makafiri wengine.

 

Na wengine wako wanaovaa pete za vito kwa maelekezo ya waganga wachawi, kukiwa na itikadi za kishirikina ndani yake. Kwa wenye kufanya hivyo, maelezo yamo kwenye viungo vifuatavyo:

 

14-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kuvaa Kitu Kwa Ajili Ya Kinga

13-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Kutundika Kitu Kwa Ajili Ya Kinga/Kumlinganisha Allaah 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share