Kaimati Za Shira Ya Karameli
Kaimati Za Shira Ya Karameli
Vipimo
Unga vikombe 2
Maji kikombe ½
Hamira 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia vitu vyote katika bakuli uchanganye vizuri unga. Acha uumuke
- Weka mafuta katika karai yashike moto vizuri kisha teka mteko mdogo mdogo ukaange vikaimati.
- Epua vichuje mafuta.
- Panga katika sahani kisha nyunyizia karamel kisha ukipenda nyunyizia kidogo kastadi (custard)
Upishi wa karamel unapatikana hapa:
Utengenezaji Wa Caramel Ya Sukari Na Maziwa ya Malai Whipping Cream
Utengenezaji Wa Caramel Au Tofi Kwa Maziwa Mazito
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)
