Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Waarabu Hawatofanikiwa Kuwaondosha Mayahudi Hadi Watekeleze Uislamu Katika Nafsi Zao
Waarabu Hawatofanikiwa Kuwaondosha Mayahudi
Hadi Watekeleze Uislamu Katika Nafsi Zao
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
“Vyovyote watakavyojaribu Waarabu, na vyovyote watakavyoijaza dunia kwa maneno na malalamiko, hakika wao hawatoweza kufanikiwa abadan kuwaondosha Mayahudi humo (katika ardhi ya Palestina) hadi kwa (njia) wito wa Dini ya Uislamu.
Na hilo kadhaalika, halitoweza kupatikana hadi kwanza wao wenyewe wautekeleze huo Uislamu katika nafsi zao.
Hakika wao watakapofanya hivyo, basi patapatikana kwao lile alilolieleza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hakitosimama Qiyaamah hadi Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu wawaue Mayahudi mpaka ifikie (abaki) Yahudi (mmoja) ajifiche nyuma ya jiwe (kubwa) na (au) nyuma ya mti. Na jiwe liseme au mti useme: “Ee Muislamu, ee mja wa Allaah, huyu Yahudi (kajificha) nyuma yangu, njoo umuue.” Al-Bukhaariy na Muslim]
Basi (ifahamike) kuwa mti, na jiwe vinawajulisha Waislamu alipo Yahudi, vinasema: “Ee mja wa Allaah”, kwa jina la uabudiwa wa Allaah (si kwa Uarabu), na vinasema: “Ee Muislamu”, kwa jina la Uislamu (si kwa Uarabu); na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Atapigana Muislamu na Yahudi, na hajasema: “Waarabu”.
[Tafsiyr Suwrat Al-Baqarah Libn ‘Uthaymiyn, mj. 1, uk. 169-170]
Alhidaaya.com