Imaam Ibn Al-Qayyim: Mapendekezo Ya Tawassul Kwa Suwrah Al-Faatihah
Mapendekezo Ya Tawassul Kwa Suwrah Al-Faatihah
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
“(Suwrah Al-Faatihah) ni ufunguo wa Kitabu na Mama wa Kitabu na Aayah saba zinazokaririwa, na shifaa kamili na dawa ya kunufaisha, na ruqya kamili, na ufungo wa utajiri na kufaulu, na hifadhi ya nguvu, na kinga ya dhiki na ghamu na khofu na huzuni kwa mwenye kuijua thamani yake na akaipa haki yake na akautumia vizuri uteremsho wake (Al-Faatihah) kwa ugonjwa wake na akajua njia ya kuiombea shifaa na kupata dawa kwayo na ni siri ambayo imekusudiwa kwa ajili yake….” [Zaad Al-Ma’aad (4/318)]