Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Maulidi: Ingelikuwa Maulidi Jambo Alipendalo Allaah Na Rasuli Lingewekewa Shariy’ah Na Kuhifadhiwa
Ingelikuwa Kusherehekea Maulidi Ni Jambo Alipendalo Allaah Na Rasuli, Lingewekewa Shariy’ah Na Shariy’ah Hiyo Ingehifadhiwa
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ingelikuwa kusherehekea Mawlid ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni katika mambo Ayapendayo Allaah Na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi yangeliwekewa Shariy’ah, na yangelikuwa yamewekewa Shariy’ah, basi ingehifadhiwa. Kwa sababu Allaah (Ta’aalaa) Amesimamia kuihifadhi Shariy’ah.
Na ingelikuwa imehifadhiwa, wasingeliacha Makhalifa Waongofu na Maswahaba Na Taabi’iyna (Waliowafuata) kwa wema na waliowafuata baada yao.
Na ambalo nawanasihi ndugu zetu Waislamu kwa ujumla, ni kwamba wajiepushe na mambo haya ambayo hayakupokewa kwao Shariy’ah yake si katika Kitabu cha Allaah wala katika Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala katika ‘amali za Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum).
Na wachunge na kuyapa uzito yale yaliyowabainikia ya wazi yaliyo katika Shariy'ah katika mambo ya faradhi na Sunnah zinazojulikana. Na hayo yanawatosha na ni katika usalama wa mtu na usalama wa jamii.
[Fataawaa Shaykh Ibn ‘Uthyamiyn (1/126)]