Kuku Wa Karai (Pakistani)

Kuku Wa Karai (Pakistani)
 
Vipimo                          

Kuku aliyekatwa vipande vipande - 5 LB

Mafuta - 1 Kikombe cha chai

Nyanya zilizokatwa ndogo ndogo - 5 kubwa

Nyanya ya kopo - 2 kiijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi (zipasue katikati) -  3 au 5

Bizari ya pilau ya unga (Jeera) - 2 vijiko vya chai

Gilgilani ya unga (Dania) - 1 kijiko cha chai

Paprika -  1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano ya unga - 2 vijiko vya chai

Chumvi -  kiasi

 Kotmiri iliyokatwa ndogondogo - 1 kikombe kimoja

Pilipili mboga (kijani) - 1

Ndimu - 2 vijiko vya supu.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Tia mafuta katika karai yashike moto vizuri.
  2. Tia Thomu na tangawizi kaanga kidogo tu.
  3. Tia nyanya, pilipili mbichi, nyanya ya kopo na bizari zote.
  4. Mtie kuku na mkaange katika masala hayo.
  5. Funika karai na wacha moto wa kiasi, kuku atoe maji yake na  apikike.
  6. Karibu na kuwiva kuku tia pilipili mboga iliyokatwa vipande vipande, kotmiri na ndimu.
  7. Funua karai na endelea kukaanga mpaka awe anakaribia kukauka,  muepue na tayari kuliwa.

 

Share