Kamba Katika Sosi Ya Nazi

Kamba Katika Sosi Ya Nazi

Vipimo 

Kamba- 1 au 2 Pakiti

Chumvi - Kiasi

Mafuta- ¼ Kikombe

Bizari ya pilau (cummin) nzima - ½ Kijiko cha chai

Vitungu- 2 Vikubwa

Nyanya zilioiiva - 3

Nazi ya kopo au ya unga - 2 Vijiko vya  supu

Siki au ndimu - 2 Vijiko vya supu

Pilipili  mbichi  iliyosagwa - 2 Vijiko vya chai

Vitungu vya kijani ( spring onions) - 3 Miche  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika    

  1. Osha kamba kwa maji ya baridi katika chungio, kisha weka  chumvi kiasi na iweke kwa firiji.
  2. Katika karai, weka mafuta yapate moto, tia bizari ya pilau lakini usiache ikaunguwa.
  3. Kisha tia vitungu na ukaange hadi zibadilike rangi ya hudhurungi lakini zisiungue.
  4. Halafu tia nyanya, tui la nazi , siki, pilipili na chumvi na iache motoni hadi nyanya zivurujike.
  5. Ongezea vitunguu vya kijani na ukoroge.
  6. Kisha tia kamba na uzipike hadi zibadilike rangi na kuiiva.
  7. Pakuwa na itakuwa tayari kwa kuliwa na wali au na mkate upendayo.  

 

   
 

Share