Mchuzi Wa Nazi Wa Nguru Na Bamia

Mchuzi Wa Nazi Wa Nguru   Na Bamia 

  

Vipimo Vya Samaki Wa Nguru  

Samaki nguru - 5 vipande 

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa- 1 kijiko cha supu 

Pilipili mbichi iliyosagwa - kijiko cha supu 

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi -1  kijiko cha chai  

Ndimu - 2 kamua maji 

Chumvi -  kiasi  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Nguru

  1. Changanya vitu vyote katika kibakuli ufanye masala ya kupaka kwenye samaki.
  2. Roweka kwa muda nusu saa
  3. Paka treya mafuta, kisha mpange nguru na mchome katika oveni.
  4. Atakapoiva upande upande mmoja mgeuze upande wa pili huku unanyunyizia mafuta.
  5. Epua weka kando.  

Vipimo Vya Mchuzi Wa Nazi  

Vitunguu maji -  2

Nyanya -   2 

Tuwi zito la nazi - 2 vikombe viwili 

Bamia - 1 kikombe  

Haldi (bizari ya manjano) -  ¼ kijiko cha chai 

Pilipili mbichi - 1 

Ndimu - kiasi 

Chumvi -  kiasi  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mchuzi

  1. Katika sufuria tia tuwi kikombe kimoja, kisha tia bamia ulizokatakata zipike ziwive kidogo.
  2. Saga kitunguu, nyanya na pilipili mbichi katika mashine ya kusagia (blender) kisha mimina katika tui la bamia.
  3. Tia vipande vya nguru, bizari, chumvi, ndimu, kisha tia tui lilobakia.
  4. Acha mchuzi uchemke kidogo kidogo kisha epua utie katika bakuli ukiwa tayari.

 

 

 

Share