Swalah Maaulum Ya Jumatano Ya Mwisho Mfungo Tano (Swafar)
SWALI:
Assalamu alaykuom,
Nasikia kuna sala ambayo inasaliwa jumatano ya mwisho ya mfungo tano je sheikh ni kweli ipo sala hiyo naomba majibu yenu, la pili
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa suala lako kuhusu Swalah hiyo ya mwezi wa Swafar au Mfungo tano. Swalah kama Ibaadah ina masharti muhimu na ya msingi ambayo yamewekwa na sharia. Ibaadah yoyote kuwa sahihi na sawa ni lazima yatimize masharti hayo:
1. Nia nzuri na Ikhlaas katika kutekeleza Ibaadah yoyote.
2. Ifuate kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Swalah za faradhi zinaeleweka barabara na vile vile zile Swalah za Sunnah kutoka katika Hadiyth zilizohifadhiwa na sahihi. Miongoni mwa Swalah za Sunnah ni zile za kabla ya Swalah ya Faradhi, baada yake, Dhuhaa, Taraawiyh, Tahajjud, Witri, na kadhalika. Hizi zote zimenukuliwa na Hadiyth zilizo sahihi. Hii Swalah ambayo umeitaja haipo kabisa ima katika zile ambazo hazikusisitizwa au zile ambazo zimehimizwa.
Hivyo, huo ni uzushi na sisi kama Waislamu hatufai kabisa kufuata mambo ambayo hayamo katika Dini yetu tukufu. Ufupi wa maneno ni kuwa hakuna Swalah kama hiyo.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
