Kusherehekea Anniversary Inafaa Kwa Waislamu?

 

Kusherehekea Anniversary Inafaa Kwa Waislamu?

 

 www.alhidaaya.com

 

 

SWALI

 

Assalam alykum.... nilikuwa nataka kuulizaa swali juu ya Annivasary....

je waislamu inafaa kusherekea annivassary? ama haifai? shukran

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Uislamu ni Dini yenye kutuongoza katika mfumo mzima wa maisha hapa duniani. Kwa ajili hiyo, lolote tufanyalo ni lazima liambatane na Shariy’ah ya Uislamu.

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwakuta watu wa Madiynah wakisherehekea siku kuu zao. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia kuwa wao wamebadilishiwa hizo sikukuu zao kwa siku mbili kuu zilizo bora kabisa, nazo ‘Iyd al-Fitwr na Al-Adhw-haa.

 

Ama sherehe ya anniversary hata ya Nabiy mwenyewe (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haipo katika siku za sherehe.

 

Ama hizi anniversaries  ambazo tunasherehekea ni katika ada na desturi za makafiri na mushrikina. Na kwa hilo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza katika Hadiyth:

 

 عن إبن عمر ((من تشبه بقوم فهو منهم)) ابن حبان - صحيح

Kutoka kwa Ibn 'Umar ((Mwenye kujifananisha na watu naye ni kama wao)) [Ibn Hibbaan ikiwa swahiyh]     

 

Na zimezuka anniversaries nyenginezo mbali na ya ndoa ambayo ndio iliyoanzishwa mwanzo na makafiri. Kumezuka  mpaka anniversary za kifo.  Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:

 

Hukmu Ya Kumbukumbu Ya Kifo (Death Anniversary)

 

Kwa hiyo, haifai kusherehekea anniversary ya tukio lolote lile.  

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share