Maulidi: Kusoma Maulidi Katika Sherehe Za Ndoa Inafaa?
Mawlid: Kusoma Maulidi Katika Sherehe Za Ndoa Inafaa?
SWALI:
Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam
Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu.
Je kufanya sherehe kama kusoma maulidi wakati wa ndoa ni halali?
Natanguliza shukrani zangu kwa Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa na nyinyi pia ndugu zetu wa Alhidaaya. Wabillah Tawfiq
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Ukisoma katika mafunzo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) utaona kuwa hakuna uzushi wa kusoma Mawlid ndani ya ndoa, na yote yanayohusiana na ndoa utayapata ndani ya vitabu hivi viwili muhimu sana katika mas-ala hayo:
Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika (Aadabu Az-Zafaaf Fiy As-Sunnat Al-Mutwahharah)
Kusoma Maulidi Kwenye Harusi Badala Kupiga Ngoma Inafaa?
Sherehe Za Harusi Zina Maasi Ya Mchanganyiko, Uzushi Wa Maulidi, Nyimbo Na Kujifakharisha
Yanayopasa Na Yasiyopasa Kutendeka Katika Ndoa
Yanayompasa Bwana Harusi Na Bibi Harusi Siku Ya kufunga Ndoa
Na Allaah Anajua zaidi